VITA WAISLAMU NA WAKRISTO GEITA, CHANZO UCHINJAJI WA MIFUGO

Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde kupitia WAPO Radio FM, znaeleza kuwa huko mkoani Geita, kuna vita kati ya Waislamu na Wakristo, kufuatia hatua ya Wakristo kuchinja mifugo kwa nia ya kuuziana wenyewe kwa wenyewe kwenye bucha walilotenga.


Jambo hilo linaelezwa kuzua tafrani kwa jamii ya Waislamu, kwani waliamua kuvamia eneo hilo na kuharibu bucha, pikipiki eneo hilo, na kusababisha watu kuingilia, na vita kuibuka, silaha za jadi zikitumika.

TUKIO:
Wakristo Mkoani Geita eneo la Katoro na Buselesele, waliamua kuachana na kununua nyama katika bucha za kawaida kwa madaikwamba hiyo ni ibada kwa waislamu, na hivyo wao hawako tayari kushiriki ibada hiyo, na badala yake watafanya ya kwao. Ndipo walipokwenda Kituo cha Polisi na kuomba kibali cha kuchinja, ambacho walipewa ilmradi wasiuze nyama hiyo.

hatimaye Wakrsito hao wakachinja na kuamua kupeleka kwenye bucha lao ambalo wamelitenga kwa ajili ya waumini wao kununua. Waislamu kuona hivyo, ndipo wakaenda kuripoti kituoi cha Polisi, na wakati Polisi (wachache) wanaongea na viongozi wa Kikristo eneo hilo ili kutatua na kurejesha amani, ndipo kundi la Waislamu likaja na kuanza kushambulia kilichokkuwa eneo hilo, wakivunja bucha, na pikipiki ya mkristo mmojawapo iliyokuwa eneo hilo.

Hatua hiyo imeelezwa kuibua hasia na kupelekea baadhi ya wat waliokuwa eneo hilo kuanza kujibu mashambulizi hayo, na mpaka hivi sasa inaripotiwa kuwa nguvu zaidi ya Jehi la Polisi haijafika eneo hilo, huku waumini wawili wa dini ya Kiislamu wakiwa katika hali mbaya kutokana na kipigo.

Silaha ni za jadi, na eneo hilo haliko salama kwa hivi sasa, kwani hata amduka mengine yamefungwa kuhofia usalama wa mali na maisha.

Akihojiwa na Beatrice Kamanga, katibu wa umoja wa makanisa ya Katoro na Buselesele, Mchungaji Silvanus Dominick, ameeleza kuwa kama hali haitatulizwa mara moja basi eneo hilo laweza kuleta madhara zaidi.

Endelea kufuatilia, nasi tutakuhabarisha kile ambacho kinaendelea kadri ambacyo taarifa zitatufikia. na pia unaweza kufuatilia kupitia WAPO Radio FM kwa kuisikiliza kwenye blog hii na tovuti ya WAPO.

ZILIZOFIKA HIVI PUNDE:

Taarifa za hivi punde ni kuwa kuna Mchungaji ameuwawa kwa kushambuliwa na silaha mbalimbali ikiwemo mawe. Halikadhalika pia kuna msikiti ulichoma moto hapo awali. Endelea kufuatilia kupitia WAPO Radio FM.

Related

VURUGU 1999641456382952281

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item