UYUI WAPOKEA MAHINDI YA MSAADA

mkuu wa wilaya ya Uyui

Halmashauri ya wilaya ya UYUI mkoani TABORA imepokea tani 480 za mahindi ya msaada kwa ajili ya wananchi waliokumbwa na njaa katika kata 13 kati ya 24 za halmashauri hiyo.
Akitoa taarifa ya msaada wa mahindi hayo Afisa Kilimo na Ushirika wa wilaya ya UYUI, Bwana TIMOTH MITIMINGI amesema kuwa tani 400 za mahindi zimekwishapokelewa na kusamabazwa katika kata 11 za wilaya hiyo.
Amesema kuwa tani 80 zinatarajiwa kuwasili wakati wowote kuanzia sasa na tani hizo zinatarajiwa kugawiwa katika kata mbili ambazo ni lutende na kizengi ambapo kila kata itapata tani 40.
Bwna MITIMINGI amesema kata ambazo zimepewa msaada wa mahindi hayo ni KIGWA,IGALULA,GOWEKO, NSOLOLO, ILOLANGULU, MABAMA,NSIMBO,SHITAGE, BUKUMBI,ISIKIZYA na, MAGIRI.
Kata za LUTENDE na KIZENGI zinatarajia kupata mahindi katika awamu ya pili pamoja na kukamilisha mgao wa mahindi kwa kata za GOWEKO, BUKUMBI na MAGIRI.
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya UYUI wametaka mfumo wa ugawaji wa mahindi ya msaada utoe kipaumbele katika maeneo yenye matatizo ya barabara wakati wa masika.




Related

UYUI 9212436668593008410

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item