AFRICAN SEVEN NATURAL WONDERS-MLIMA KILIMANJARO, NGORONGORO CRATES NA MBUGA YA SERENGETI
https://menacotz.blogspot.com/2013/02/african-seven-natural-wonders-mlima.html
Waziri Mkuu Mizengo
Pinda akipiga makofi mara baada ya kumkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Hifadhi
za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi anayenyanyua juu juu tuzo ya Mbuga ya
wanyama ya Serengeti mara baada ya kuitangaza mbuga hiyo kuwa ni moja ya
maajabu saba ya asili katika bara la Afrika kwenye hoteli ya Mount
Meru, Kushoto ni Bw Philip Imler Mwanzilishi wa Taasisi ya Seven Natural
Wonders Bw. Philip Imler.
Tanzania imefanikiwa
kushinda kupitia vivutio vyake vitatu vya utalii ambavyo ni Mlima
Kilimanjaro, Ngorongoro Crates na Mbuga ya wanyama ya Serengeti, hafla
hiyo imehudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na
Mabalozi, Wafanya biashara,Mawaziri, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania na wadau mbalimbali wa utalii kutoka Mataifa
mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Katika picha kulia ni
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki na Lynn Imler mmja
wa wakurugenzi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders.
Waziri Mkuu Mizengo
Pinda akimkabidhi zawadi ya picha ya Ngorongoro Crates muanzilishi na
muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler mara
baada ya kumalizika kwa hafla ya kutangaza maajabu saba ya asili ya
Afrika iliyofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.Vikundi wa ngoma kutoka makabila ya mkoa wa Arusha vilipamba hafla hiyo kamavinavyoonekana.Wadau kutoka TTB ambao pia walikuwa ni miongoni mwa wanakamati ya maandalizi wakiwa katika picha ya pamoja.Mkurugenzi
wa Bodi ya Utalii TTB Dk. Aloyce Nzuki akisalimiana na Mbunge wa Jimbo
la Iringa mjini Mchungaji Msigwa, Kushoto ni Mh Shah kutoka Mafia na
mmoja wa wajumbe wa bodi ya Utalii TTB.Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania wakiwa katika hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wa dini walihudhuria pia.
Mbunge Mh. James Lembeli akisalimiana na Bw. Mike Teyrol walipokutana katika hafla hiyo.
Mwanamuziki Mrisho Mpoto na Kundi lake wakitumbuiza wakati wa utoaji wa tuzo hizo.
Mkurugenzi wa Masoko wa
Bodi ya Utalii Bi Devitha Mdachi akiwa pamoja na maafisa wengine wa bodi
hiyo wakipokea wageni mbalimbali waliofika katika hafla hiyo.
Waziri wa Maliasili na
Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Bodi
ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki.
Waziri wa Maliasili na
Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Bibi Maimuna Tarishi katikati ni msaidizi wake Bw. Miskanji.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu akiwa meza
kuu pamoja na viongozi wengine wakati wa utoaji wa tuzo hizo za Seven
Natural Wonders jijini Arusha jana jioni., kutoka kulia ni Magesa
Mulongo mkuu wa Mkoa wa Arusha, Agness Agunyu Waziri wa Utalii kutoka
nchini Uganda na kutoka kushoto ni Bw. Philip Imler kutoka Taasisi ya
Seven Natural Wonders na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis
Kagasheki.
Mkurugenzi wa Hifadhi za
taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi akiwasikiliza wabunge waliohudhuria
katika hafla hiyo kulia ni Deo Filikunjombe na kushoto ni David
Kafulila.
Waziri Mkuu Mizengo
Pinda akiongozwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Dk. Aloyce Nzuki wakati
alipowasili kwenye hoteli ya Maount Meru kwa ajili ya utoaji tuzo hizo.
Mama Tunu Pinda wa pili
kutoka kushoto akiwa katika hafla hiyo, kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya
Utalii Tanzania (TTB) Dk Aloyce Nzuki na katikati ni Lynn Imler kutoka
Seven Natural Wonders.
Mabalozi mbalimbali
waliohudhuria katika hafla hiyo wa kwanza kutoka kulia ni Balozi Mutinda
Mutiso Balozi wa Kenya Nchini Tanzania.
Waziri wa Maliasili na
Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na mbunge wa jimbo la Arusha
Mjini Bw. Godbless Lema kabla ya kuanza kwa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki akiongea katika hafla hiyo.
Bw Allan Kijazi kushpto akiwa na wadau wengine katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu Mizengo
Pinda akimkabidhi tuzo ya Hifadhi ya Ngorongoro Crates Mkurugenzi wa
Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi katika hafla hiyo, kushoto ni
Philip Imler wa Seven Natural Wonders.
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi akiongea katika hafla hiyo.
Muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler akizungumza katika hafla hiyo.
Tuzo ya mlima Kilimanjaro ikapokelewa na mhifadhi wa mlima huo kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Philip Imler kushoto.
Post a Comment