HALMASHAURI KUU YA CCM YATOA TAMKO LA VURUGU ZA MTWARA

Hili hapa chini ndio tamko la HALMASHAURI KUU YA CCM

 katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi-Nape Nnauye

TAMKO LA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM KUHUSU MAANDAMANO NA VURUGU ZILIZOTOKEA MKOANI MTWARA JUU YA UJENZI WA BOMBA LA GESI
NA MAENDELEO YA MKOA WA MTWARA

1. Halmashauri Kuu ya Taifa imepokea maelezo ya Serikali kuhusu maandamano na vurugu zilizotokea Mkoani Mtwara tarehe 27 Desemba, 2012 tarehe 25 Januari, 2013 na tarehe 26 Januari, 2013. Maandamano na vurugu hizo zilizodaiwa kuwa na lengo la kupinga mradi wa bomba la Gesi kujengwa na kupeleka Gesi Dar es Salaam.

2. Baada ya kupokea maelezo haya ya Serikali, Halmashauri Kuu ya Taifa imebaini kuwa: -

(a) Kwa sehemu kubwa Wananchi wa Mkoa wa Mtwara hawakuwa wamepewa elimu ya kutosha juu ya uendelezaji wa Gesi na jinsi watakavyonufaika.

(b) Baadhi ya Wanasiasa na baadhi ya Viongozi wa Makundi mbalimbali waliamua kutomia suala la Gesi kupandikiza lugha za chuki, uchochezi na upotoshaji wa maendeleo ya Mradi wa Gesi kwa lengo la kujitafutia umaarufu.

(c) Suala la Gesi limetumika kama kisingizio tu cha kufanya vitendo vya rurugu na uvunjifu wa amani.



3. Kutokana na ukweli huu, Halmashauri Kuu ya Taifa inaelekeza ifuatavyo:-

(i) Imesikitishwa na vurugu zilizotokea na kusababisha watu kadhaa kupoteza maisha na uharibifu mkubwa wa mali na majengo ya CCM, Serikali, Wabunge na watu binafsi. Halmashauri Kuu ya Taifa inawapa pole wafiwa na waliopoteza mali zao.

(ii) Inaiagiza Serikali kufanya uchunguzi wa kina kuhusu waliofanya vurugu na uharibifu mbalimbali na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa Sheria. Pia, kuwa makini na kuhakikisha matukio kama haya hayajitokezi tena.

(iii) Inaiagiza Serikali kuendelea kutoa elimu ya kutosha kwa Wananchi wa maeneo husika kuhusishwa na kuelimishwa juu ya miradi mbalimbali kwenye maeneo yao.

(iv) Halmashauri Kuu ya Taifa inawataka Wananchi wa Mkoa wa Mtwara kuendelea kuishi kwa amani na utulivu kama ilivyo desturi yao, maana vurugu pamoja na kuharibu mali na kugharimu maisha vinaweza kuwakimbiza wawekezaji waliojitokeza na ambao shughuli zao zitawafaidisha wananchi wa Mkoa huu na Watanzania kwa ujumla .



HALMASHAURI KUU YA TAIFA
Dodoma 10 – 11 Februari,2013

Related

Politics 7234411715416976745

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item