BREAKING NEWZZZ ... Majina ya Tume ya Waziri Mkuu ya kuchunguza Matokeo CSEE 2012 haya hapa
https://menacotz.blogspot.com/2013/03/breaking-newzzz-majina-ya-tume-ya.html
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda leo Jumamosi, Machi 2, 2013 amezindua Tume maalum
aliyoiunda ili ifanye uchunguzi wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne
yaliyotangazwa Februari 18, mwaka huu na kuwataka wajumbe wa Tume hiyo
watafute kiini cha mserereko wa kushuka kwa ufaulu kuanzia mwaka 2010
hadi 2012.
Waziri
Mkuu amezungumza na wajumbe wa Tume hiyo kwenye ukumbi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu, Magogoni, jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulihudhuriwa
pia na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa.
Amesema
kwa mujibu wa hadidu za rejea, wajumbe wa tume hiyo watatakiwa
kuangalia ni sababu zipi zimechangia kuwepo kwa matokeo hayo mabaya,
mserereko wa kushuka umekuwa ukiongezeka kwa sababu gani, usimamizi
katika Halmashauri ukoje, ukaguzi wa elimu na uhamishiwaji wa sekta ya
elimu kwenye Wizara ya TAMISEMi umechangiaje kushuka kwa kiwango cha
ufaulu.
Vilevile,
watatakiwa kuangalia mitaala na mihutasari ikoje, kuangalia uwiano
uliopo kwenye mitihani inayotungwa ikiwa ni pamoja na uhakiki wa
mitihani hiyo; kuangalia mazingira ya kufundishia, mfumo wa upimaji,
usimamizi na uendeshaji, na kutokuwepo kwa chakula shuleni
kunachangiaje kushuka kwa utendaji mbaya wa wanafunzi katika masomo
yao.
Tume
hiyo yenye wajumbe 15, imepewa muda wa wiki sita kuanzia Machi mosi
iwe imekamilisha kazi hiyo na kuwasilisha taarifa yao kwa Waziri Mkuu.
Tume
itaongozwa na Prof. Sifuni Mchome wa Tume ya Vyuo Vikuu, na Makamu
wake atakuwa Bi. Bernadetha Mushashu (Mbunge wa Viti Maalum – Kagera).
Wajumbe
wengine ni Bw. James Mbatia (mbunge wa Kuteuliwa), Bw. Abdul J.
Marombwa (Mbunge wa Kibiti), Prof. Mwajabu Possi (Chuo Kikuu - UDSM),
Bibi Honoratha Chitanda (CWT), Bibi Daina Matemu (TAHOSSA) na Bw.
Mahmoud Mringo (TAMONGSCO).
Post a Comment