MOSHI MWEUSI WAFUKA VATICAN KUASHIRIA KUWA BADO PAPA HAJAPATIKANA....



Moshi mweusi ulifuka jana jioni kutoka kwenye dohani huko Vatican ikiwa ni ishara kwamba Baraza la siri la Makadinali bado halijampata Kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki baada ya kupiga kura ya kwanza.

Mchakato wa kupiga kura ulianza mapema jana ambapo Makadinali 115 kutoka nchi 48 walikutana kwa faragha ili kumchagua atakaechukua nafasi ya aliyekuwa papa Benedikt wa 16 aliejiuzulu mwishoni mwa mwezi uliopita.


Zoezi la kupiga kura litaendelea hadi hapo mmoja wa Makadinali atakapopigiwa theluthi mbili ya kura yaani kura 77.


Atakaefikia kiwango hicho atakuwa Baba Mtakatifu wa 266.


Ikiwa Makadinali, wanaopiga kura watakubaliana juu ya Kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki, moshi mweupe utatoka dohani na kengele zitapigwa kwenye makao makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican.

Related

SIKU YA KWANZA YA PAPA FRANCIS 1

Kazi yaendelea Vatican Siku yake ya kwanza ofisini kama Papa mtakatifu wa kanisa Katoliki, Papa Francis 1 tayari anaanza kazi. Papa anatarajiwa kuwateua wafanyikazi wak...

BAADA YA DENEDICT XVI:::: Sasa ni Papa Francis I !

Papa Francis ahutubu mara ya kwanza Kadinali Jorge Mario Bergoglio wa Argentina amechaguliwa kuwa Papa mpya wa Kanisa Katoliki. K...

PAPA BENEDICT XVI ATANGAZA KUJIUZULU FEBRUARY 28

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa BENEDICT XVI anatarajia kujiuzulu madaraka hayo February 28 mwaka huu kwa mujibu wa ripoti kutoka Vatican. Msemaji wa Papa Benedict Father Fede...

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in weekRecentBLOG ZINGINE

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item