Mwalimu wa kwanza kuwa na ‘Daraja A’ Tanzania afariki dunia
https://menacotz.blogspot.com/2013/03/mwalimu-wa-kwanza-kuwa-na-daraja.html
Mwalimu
wa kwanza Tanzania wa daraja la A(Grade A) ambaye pia alikuwa ni
padre wa jimbo kuu katoliki la Songea padre John Fratera Gama amefariki
dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Marehemu
padre Gama amefariki katika hospitali ya misheni Peramiho iliyopo
kilometa 24 kutoka mjini Songea ambako alikuwa amelezwa kutokana na
kusumbuliwa na magonjwa ya moyo na kisukari.
Askofu
mkuu wa jimbo kuu katoliki la Songea mhashamu Norbert Mtega amesema
kuwa marehemu padri padre Gama atakumbukwa na watanzania wengi hasa
kutokana na vipaji vyake ikiwemo kuwa miongoni mwa walimu wanne wa
kwanza wa Tanzania waliopewa daraja la daraja A(Grade A) katika chuo cha
uliamu Tabora mwaka 1944.
"Wananchi
wa kawaida, Mapadre wengi na wahashamu maaskofu kadhaa wa ukanda wa
kusini wamelelewa na kufundishwa naye,amekuwa mwamba wa taaluma hasa
katika fani za falsafa na lugha ya kilatini alioweza kuwafundisha
wanafunzi wake kwa umahiri mkubwa’’, alisisitiza mhashamu Mtega.
Mwalimu wa kwanza wa daraja la A (Grade) Tanzania marehemu padre John Frateri Gama
Aliongeza
kuwa padre Gama alipenda kujiendeleza kitaaluma na alifarijika
kuwawezesha watanzania wengine kitaaluma kutokana na kuamini kuwa elimu
bora ni pato la kuwa na walimu bora hali ambayo ilileta mafanikio
makubwa kiutendaji katika kanisa, taasisi za umma na watu binafsi.
Historia
ya maisha yake inaonyesha kuwa afya yake ilizidi kutetereka kuanzia
mwaka 2011 kutokana na kuzidiwa na tatizo la kisukari ambalo
lilidhoofisha mwili wake na kuathiri mguu wake wa kushoto
uliowalazimisha madaktari kuukata mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu
kwa lengo la kuokoa maisha yake.
Marehemu
padre Gama ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 88 na miaka 56 ya
upadre hadi mauti yanamkuta alikuwa anatoa huduma kama mchungaji na
muhudumu wa kiroho katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma ya mjini Songea.
Marehemu
padre Gama alizaliwa Luyangweni wilayani Songea mwaka 1926,elimu ya
msingi alipata kati ya mwaka 1933 hadi 1937 katika shule za msingi
Likuyufusi na Mshangano,elimu ya sekondari kati ya mwaka 1938 hadi 1943
sekondari ya Malangali na mafunzo ya ualimu aliyapata mwaka 1944 katika
chuo cha ualimu Tabora na kutunukiwa cheti cha ualimu daraja la A.
Masomo
ya seminari aliyapata kati ya mwaka 1945 hadi 1950 seminari za
Kigonsera na seminari kuu Peramiho ambapo chuo kikuu alisoma kati ya
mwaka 1965 hadi 1967 Roma Italia katika chuo kikuu cha Angelicum na
kutunukiwa masters ya falsafa.
Padre
Gama pia mwaka 1967 hadi 1968 alisoma chuo kikuu cha Makerere nchini
Uganda na kupata stashahada ya ualimu na mwaka 1977 alisoma chuo cha
Chama Cha Mapinduzi Kivukoni jijini Dar es salaam alitunukiwa stashahada
ya siasa ya ujamaa.
Misa
ya mazishi ya mwalimu na padre Gama ilifanyika katika kanisa la
kiaskofu la mtakatifu Mathias Kalumba jimbo kuu la Songea ambayo
ilioongozwa na Askofu mkuu Norbert Mtega ambapo mazishi yaliohudhuriwa
na maelfu ya wakazi wa Songea yalifanyika katika makaburi ya parokia
ya Matogoro nje kidogo ya mji wa Songea.
Post a Comment