UPDATES KUHUSU MHARIRI ALIYEFANYIWA UKATILI ABSALOM KIBANDA..AMETOBOLEWA JICHO KWA NONDO


UPDATE/TAARIFA MPYA: KWA SASA YADAIWA KUPELEKWA SOUTH AFRICA KWA MATIBABU ZAIDI

Kwa mujibu wa maelezo ya mgonjwa aliyekaririwa akizungumza kwa shida, ameeleza kuwa, majira ya usiku wakati akiingia nyumbani kwake alivamiwa na watu watatu --mmoja akiwa ameshika bastola na wawili wakiwa wameshika nondo-- ambapo alipofika nje ya nyumba yake, watu hao walilivamia gari lake, wakauvunja mlango wa gari lake, wakamtoa nje, wakaanza kumpiga vibaya sana, wakamtoa meno mawili, wakamng'oa kucha katika moja ya vidole vyake na kumtoboa jicho lake kwa nondo.
Picture
Absalom Kibanda akiwa hospitalini
Mhariri Mkuu wa Kampuni ya New Habari wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Dimba, Bingwa na Dimba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ndugu, Absalom Kibanda amevamiwa na watu wasiojulikana akiwa ndani ya gari lake wakati akiingia nyumbani kwake  huko Mbezi-Beach, jijini Dar es Salaam.

Akielezea tukio hilo wakati akihojiwa na Radio One Stereo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya New Habari, Hussein Bashe amesema Kibanda alivamiwa majira ya saa sita usiku wa jana, akitokea kwenye majukumu yake ya kila siku. Inadaiwa kuwa alitolewa kwenye gari, akapigwa kichwani, akajeruhiwa jichoni na kisha kutelekezwa mbali kidogo ya nyumbani kwake.

Wasamaria wema waliomwona walimpeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambako alipokelewa vizuri na madaktari na kumpatia tiba ya awali na baadaye kumhamishia kwenye Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) ambako mpaka sasa anaendelea na matibabu.

Watu waliotenda ukatili huo hawakuchukua kitu chochote kwenye gari.

Taarifa za awali pamoja na picha vimetolewa na Chogolo kupitia kundi pepe la MabadilikoTanzania (bofya hapa kuendelea kusoma updates/taarifa mpya/reactions zinazotolewa kuhusiana na tukio hili).
Picture
(picha iliyopigwa na Chogoloh saa tisa usiku hospitalini Muhimbili)
Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto, alisema kuwa watu hao waliohusika wakamatwe ili sheria ichukue mkondo wake.

Tusingependa Kama waandishi kuamini yanayosemwa lakini kutokana na uadilifu mkubwa wa vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama kuwapata watu ambao wamehusika na tukio hilo.

Sisi tunaamini tukio hili la mwenzetu kuvamiwa na watu hao halikuwa kwa bahati mbaya ni Jambo ambalo linaonekana Kama limepangwa na Kama ni hivyo lengo na madhumuni yake ni nini kwa waandishi wa Tanzania? Uhuru na Usalama wa waandishi upo wapi?

Katakana na tukio hili la mpiganaji na Kiongozi wetu kuvamiwa ,ipo haja ya sisi waandishi kuungana pamoja katika kutafuta Usalama wetu.kuna matukio mengi ya waandishi yametokea na tumekuwa tukipiga kelele lakini matokeo yake hakuna hatua ambazo serikali inayafanyia kazi.

Katakana na majeraha maki wa aliyopata mwenzetu,tunaiomba serikali na hats Mheshimiwa Rais,Dr Jakaya Kikwete kutoa Masada wa mwenzetu kwenda kutibiwa nje,tunaamini serikali ni sikivu na Rais wetu ni mwenyeji kusikia kilio cha watu wake.

Kibanda na wenzak ndani ya Jukwaa la wahariri wamekuwa mstari wa mbele katika kurudisha hadhi ya tasnia ya habari na kujenga umoja miongoni mwa waandishi wa habari na kuifanya tasnia ya habari kuheshimika tofouti na ilivyokiwa nyuma.

Tunaungana na kampuni ya habari, wafanayakazi wenzak, familia yake na waandishi wote kwa jumla na kumuomba mungu ampomye ili tuweze kuunganae nae katika kusaidia kupasha habari Watanzania lakini ili aweze kuwaongoza waandishi wenzake.

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2MkyAtJXA

Related

BREAKING NEWZ 4915397478795137705

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item