ARSENAL. CHELSEA ZASHINDA, LIVER, SPURS, EVERTON, QPR, WIGAN ZATOKA SARE LIGI KUU YA UINGEREZA
https://menacotz.blogspot.com/2013/04/arsenal-chelsea-zashinda-liver-spurs.html
Meneja
mpya wa SUNDERLAND PAULO DI CANIO jana ameanza vibaya kibarua chake
baada ya kushuhudia THE BLACK CATS wakifungwa bao 2 kwa dhidi ya wenyeji
wao CHELSEA licha ya SUNDERLAND kuanza kuongoza kupata bao.
Kipigo hicho kinaifanya SUNDERLAND kuwa katika nafasi ya 17 kwa pointi 31 sawa na timu ya WIGAN iliyopo katika nafasi ya 18 ikiwa ni nafasi ya hatari ya kushuka daraja nayo ikiwa na pointi 31.
SUNDERLAND walianza vizuri mchezo huo kwa kupata bao kwenye dakika ya 45 pale CESAR AZPILIKUELTA alipotumbukiza mpira kwenye nyavu za lango ya timu yake.
Lakini katika kipindi cha pili CHELSEA walisawazisha bao hilo kwenye dakika ya 47 baada ya beki wa SUNDERLAND MATT KLIGALLON kujifunga mwenyewe.
Kwenye dakika ya 55 CHELSEA walikua mbele kufuatia BRANISLAV IVANOVIC kuugusa mpira uliopigwa na DAVID LUIZ na kuubadilisha uwelekeo ambapo ulimpoteza kipa na kujaa wavuni.
Aidha meneja wa muda wa CHELSEA RAFA BENITEZ amesema kuwa walilazimika kujiimarisha katika kipindi cha pili na kuongeza kuwa kitu kibaya katika ule mchezo ni kwamba wameruhusu kufungwa goli na kitu kizuri ki kuwa walifanikiwa kurudisha na kushinda.
Michezo mingine iliyochezwa jana, TOTTENHAM HOTSPURS ikiwa kwenye uwanja wa nyumbani imetoka sare ya kufungana mabao MAWILI kwa MAWILI na EVERTON.
Majogoo wa jiji LIVERPOOL nao wameshindwa kutamba nyumbani kwao ANFIELD baada ya kuambulia suluhu na wagonga nyundo wa LONDON WESTHAM UNITED na timu zinazopingania nafasi ya kutoshuka daraja QPR imetoka sare na WIGAN ATHLETIC.
===
Katika mashindano ya LANGALANGA bingwa mtetezi JORGE LORENZO amefanikiwa kuanza vizuri mashindano ya ufunguzi baada ya kushinda nchini QATAR.
Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 25 alianza kuongoza kuanzia mwanzo na kufanikiwa kuwazidi wapinzani wake na kuweka rekodi ya ushindi wake wa 24 kwenye mashindano hayo.
Nyuma ya LORENZO kulikua na ushindani wa madereva wanne ambapo VALENTINO ROSSI ndiye aliyeshinda nafasi hiyo ya pili akiwa amerejea kwenye YAMAHA.
Dereva ambaye ndiye ameanza mashindano hayo jana MARC MARQUES alikamata nafasi ya 3 huku dereva mwenzake wa timu moja DANI PEDROSA akikamata nafasi ya nne wakati mwingereza CARL CRUTCHLOW akichukua nafasi ya tano.
LORENZO aliwashinda wenzake kwa karibu sekunde 6 lakini alikua ni VALENTINO ROSSI ambaye kiwango chake ndio kitakua gumzo kubwa pale alipotoka kwenye nafasi ya 5 hadi ya pili huku zikiwa zimesalia lap 10 mbio hizo kumalizika.
Dereva huyo mwenye miaka 34 alikua kwenye timu ya DUCATI kwa miaka 2.
ROSSI alianza vibaya mashindano hayo ambapo alitoka nje ya barabara na kukamata nafasi ya saba lakini alifanikiwa kurudi hadi nafasi ya tano ambapo aliwapita CRUTCHLOW na PEDROSA na kukamata nafasi ya pili.
= = = = = = ==
Katika tenesi ,Novak Djokovic ameipeleka SEBIA katika nusu fainali ya michuano ya kuwania kombe la DAVIS baada ya kumfunga Sam Querrey wa MAREKANI kwa seti tatu kwa moja ya 7-5, 6-7, 6-1, 6-0 katika mchezo wa robo fainali.
Robo fainali nyingine imeshuhudia ARGENTINA ikiifunga UFARANNSA kwa ushindi wa TATU kwa MOJA mijini Buenos Aires wakati mabigwa watetezi JAMHURI ya CHEKI nayo ikitinga hatua ya NUSU FAINALI baada ya kuifunga Kazakhstan kwa TATU kwa MOJA mjini ASTANA.
MUARGENTINA, Juan Monaco alimtandika MFARANSA WILFRIED TSONGA kwa ushindi wa 6-3, 6-3, 6-0.
POLAND nayo imetinga katikaa hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga AFRIKA KUSINI kwa TATU kwa moja
Katika mchezo huo Jerzy Janowicz wa POLAND alimfunga Ruan Roelofse wa AFRIKA KUSINI kwa ushindi wa 4-6, 6-3, 6-1, 6-1
====
Mchezaji namba moja kwa ubora wa tenesi dunia kwa upande wa wanawake SERENA WILLIAMS amenyakua ubingwa wa FAMILY CIRCLE CUP na baada ya kumfunga JELENA JANKOVIC kaatika mchezo wa fainali.
Huu unakuwa ni ubingwa wa 49 kwa SERENA WILLIAMS,na katika mchezo huo alishindaa kwa seti mbili kwa moja ya 3-6, 6-0, 6-2 .
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo Williams amesema amefurahi kuteta ubingwa wake japo mchezo huo wa fainali ulikuwa mgumu.
====
Katika gofu mchezaji namba mbili kwa ubora wa gofu dunia ROYI MAKAROYI ameshindwa kutamba katika michuano ya wazi ya TEXAS baada ya kufungwa na Martin Laird kutoka SCOTLAND kwa mikwaju 63.
Katika michauno hiyo Martin Laird alimaliza michuano hiyo kwa jumla ya mikwaju 274 wakati MAKAROYI 276.
Billy Horschel alimazika katika nafasi ya tatu akiwa amepinga mikwaju 277 na K.J. Choi kutoka KOREA amemaliza katika nafasi ya nne baada ya kupinga jumla ya mikwaju 279 .

Posted by
MENACO
Post a Comment