KUMBUKUMBU YA MWAKA MMOJA TANGU KUFARIKI MSANII STEVEN KANUMBA
https://menacotz.blogspot.com/2013/04/kumbukumbu-ya-mwaka-mmoja-tangu.html
Steven
Kanumba akiwa katika ofisi za Global Publishers baada ya kurudi kutoka
Afrika Kusini katika jumba la BBA Septemba 11, 2009.
Kanumba
akihojiwa na Sauda Mwilima (kushoto) alipokwenda kutoa msaada katika
kituo cha watoto yatima cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza jijini Dar es
Salaam, Agosti 2011.
Steven
Kanumba akiwa na furaha baada ya kupokelewa Uwanja wa Ndege akitokea
nchini Afrika Kusini alipokuwa amealikwa kama staa katika jumba la BBA
Septema 9, 2012.
Kanumba
akisalimiana na Mzee Kipara alipomtembelea nyumbani kwake Kigamboni,
Septemba 2010. Wasanii wote wawili kwa sasa ni marehemu.
Staa
wa filamu kutoka Nigeria, Ramsey Noah, akiongea na wanahabari baada ya
kuwasili nchini kushiriki katika filamu iliyopewa jina la Devil’s
Kingdom ambayo iliandaliwa na Kanumba (pembeni), Aprili 2011.
Steven Kanumba (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Paradise Hotel Justuce Bagumu (kushoto) na Ramsey Tokumbo Nouah (katikati) ndani ya ukumbi wa Paradise Hotel
wakati wa hafla ya kumuaga Ramsey baada ya kukamilisha filamu ya
Devil's Kingdom, iliyoandaliwa na kampuni ya Kanumba The Great Films
Production Aprili 2011.
LEO ni mwaka tangu msanii maarufu wa filamu Bongo, Steven Charles
Kanumba kuiaga dunia. Marehemu Kanumba alifariki dunia alfajiri ya
Jumamosi Aprili 7, 2012 akiwa na umri wa miaka 28, baada ya kile
kilichodaiwa kuwa ni ugomvi wa kimapenzi na rafiki yake wa kike,
Elizabeth Michael kwa jina maarufu “Lulu” na kuzikwa Aprili 10, 2012 na
maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na wengineo.Mpaka sasa bado hajatokea msanii wa kuziba pengo aliloliacha marehemu katika tasnia ya filamu. Pichani juu ni baadhi ya taswira za marehemu enzi za uhai wake zilizochukuliwa na mtandao huu.
Mungu ailaze roho ya marehemu Steven Charles Kanumba mahali pema peponi.
Post a Comment