TAKUKURU YAWAFUNGULIA WACHEZAJI WA AZAM FC>>>>>>> WADAI TUHUMA HAZIJATHIBITISHWA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA

S. L.P. 42325,
Temeke,
Simu: 022 2850633,
Nukushi: (022) 2850635,
Baruapepe:rbctemeke@pccb.go.tz,
Mtandao www.pccb.go.tz

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UCHUNGUZI WA WACHEZAJI WA TFF
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inatoa taarifa kwa umma kwamba, uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU Mkoa wa Temeke dhidi ya wachezaji wanne wa timu ya soka ya AZAM waliokuwa wakituhumiwa kupokea hongo/rushwa ili kupanga matokeo, haukuweza kuthibitisha tuhuma hiyo.

Kosa la kupokea rushwa ni kinyume na Kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007. Kwa mujibu wa kifungu hicho ni kosa kwa mtu yoyote kuomba, kupokea, kushawishi au kulazamisha kupewa rushwa au kuahidi kutoa rushwa.

Wachezaji waliokuwa wakilalamikiwa ni (1) DEOGRATIUS BONIVENTURE MUSHI (DIDA), (2) ERASTO NYONI, (3) SAID HUSSEIN MORAD na (4) AGGREY MORRIS. Wachezaji hawa kwa pamoja walituhumiwa kupokea rushwa kwa lengo la kupanga matokeo ya mechi kati ya AZAM FC na SIMBA SPORTS CLUB iliyochezwa tarehe 27/10/2012 katika Uwanja wa Taifa – jijini Dar es salaam. Katika mechi hiyo AZAM FC ilifungwa magoli 3 - 1.


Tuhuma hizo ziliwasilishwa TAKUKURU Mkoa wa Temeke tarehe 9/11/2012 kutoka AZAM FC ikiwatuhumu wachezaji hao kupokea kiasi cha shilingi milioni saba (7,000,000/=) kutoka kwa uongozi wa Simba Sports Club ili wagawane na kupanga matokeo ya mechi. Fedha hizo zilidaiwa kupokelewa siku moja kabla ya mechi kati ya AZAM FC na SIMBA SC (tarehe 26/10/2012).

AZAM FC, imeweza kutimiza wajibu wake wa kushiriki katika kuzuia na kupambana na rushwa kwa kutoa taarifa za tuhuma za rushwa kwa TAKUKURU – chombo ambacho ndicho chenye dhamana na mamlaka ya kisheria kuchunguza makosa ya rushwa.

Tunatoa wito kwa taasisi nyingine na wananchi kwa ujumla, kuendelea kutoa taarifa za tuhuma za rushwa kwa TAKUKURU ili kwa pamoja tuweze kudhibiti vitendo vya raushwa katika nchi yetu


Imetolewa na Doreen J. Kapwani - 
Afisa Uhusiano wa TAKUKURU, Jumatatu tarehe 08/04/2013

Related

AZAM FC 7681330984048305566

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item