RIWAYA: PAINFUL TRUTH (UKWELI WENYE KUUMA)----------3

 

MTUNZI: Nyemo Chilongani

MAWASILIANO: 0718 06 92 69

SEHEMU YA TATU

“Nitachagua wa kumuoa hapo baadae. Ila hata Happy nae anafaa sana. Mmh! Wazazi watanielewa vipi kama nikimuoa? Kwanza hawamjui hata mara moja, wataweza kuniunga mkono katika maamuzi yangu? Mmh! Huo nao uamuzi mgumu” Wayne alijisemea wakati ndege ikiwa imekwishafika katika ardhi ya Morocco tayari kwa kuendelea na safari ya kuingia Ulaya na kisha kuelekea Marekani. Jina la Brown Michael Ryn lilikuwa jina kubwa miongoni mwa matajiri ambao walikuwa wakipatikana nchini Marekani. Mzee huyu alikuwa akimiliki miladi mikubwa nchini Marekani pamoja na mingine iliyokuwa katika mataifa makubwa kama Uingereza, Urusi na Ufaransa. Huyu ndiye alikuwa mwasisi wa shirika la ndege la American Airways, ndiye alikuwa akimiliki kiwanda kikubwa cha kutengeneza makaratasi cha Brown Paper Company Limited, huyu ndiye ambaye alikuwa akiimiliki kampuni kubwa ya kutengeneza magazeti ya Independent ambayo yalikuwa yakitoka mara mbili kwa wiki nchini Marekani. Tofauti na vitega uchumi hivyo, pia alikuwa na kampuni nyingi pamoja na visima vya mafuta nchini Qatar. Jina lake lillikuwa kubwa na kila siku alikuwa akiingiza kiasi kikubwa cha fedha katika maisha yake. Mpaka inafika mwaka huo wa 1990, Bwana Brown alikuwa ameingiza kiasi cha dola bilioni sabini katika mwaka huo na kumfanya kuwa tajiri namba kumi na nane duniani. Maisha yake siku zote yalikuwa yametawaliwa na fedha, alikuwa akithamini sana fedha kuliko kitu kingine chochote kile.
ENDELEA HAPA>>>>>>>>>>>>>

Related

HADITHI 3463257386262671004

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item