RIWAYA: MREMBO ALIYEPOTEA--------------------6
https://menacotz.blogspot.com/2013/04/riwaya-mrembo-aliyepotea.html
MTUNZI: Andrew Carlos
MAWASILIANO: 0713133633
SEHEMU YA SITA
Taratibu John akaanza kufungua jicho lake moja na baadaye likafuatia jngine na sasa akawa anaangaza huku na kule nakushangaa watu waliokuja kumuona.
“Mke wangu yuko wapi? Angel wangu yupo wapi nimesema?”
John alishtuka nakuanza kumtaja Angel hali iliowafanya kila mmoja wa marafiki zake kumshangaa hadi mkewe wakajua atakuwa amechanganyikiwa na kukosea kwa kumtaja Angel badala ya mkewe Janet. Akili ya Janet sasa ikawa ni kuhakikisha mumewe anajua kuwa yupo pale nakuwa amrekebishe mumewe asimtaje Angel amtaje Janet.
“Mume wangu?, nimekuja ni mimi Mkeo Janet, amka ule?”
“Hapana najua wewe ni Janet lakini namtaka Angel wangu sasa hivi”
“Angel ndio nani?, kwanza Angel hayupo hapa yupo kwao hukoo!”
Janet alijikaza bila ya kujua angel anayezungumziwa na John hivyo akaona kama amemdanganya atatulia tu.
“Jamani sitaki mivyakula yenu namtaka Angel nimesema?, Kwanza Alice nayeye amepona? yupo wapi?”
Hasira kali zilizoambatana na wivu ndani yake zikaanza kujijenga kichwani mwa Janet, Ule uvumilivu aliokuwa ameuonesha toka mwanzo ukawa sasa umeisha. Akaona dunia chungu kwa muda, Hakuamini kama mumewe John yupo siriazi kwa kutaja hao wanawake asiyewajua hata kwa sura. Akafikiria mengi sana mpaka akajiona hana thamani hata kwa mwanaume yeyote, aliamini kila rafiki yake aliyekuja kumtembelea atakuwa anajua matatizo yake ya kutokuzaa hivyo hata hao anaowataja John watakuwa wanamjua ila wanamficha tu. Akaamua kujishusha kama mwanamke aliyefundishwa na wazazi nakuanza kumbembeleza John ale kwa mara nyingine.
“Mume wangu John!, kula basi halafu ndio uongee hayo mambo mengine!”
“Hivi hamnisikii heee, wewe nimesema sikutaki tena maishani mwangu, na ni mmoja tu aliokuwa amebeba mimba yangu na nilimpenda sana, Angel!! Yes! Angel!! nipelekeni nikamuone”
John hasira zilimpanda zaidi akachukuwa bakuli ambalo tayari Janet alikuwa amemimina zile ndizi na kumwaga chini, Kisha akajitoa ile dripu aliokuwa amefungwa nakuinuka.
“Haya namtaka Angel wangu sasa hivi?, Na pia nataka nimuone Alice?”
Ule uvumilivu ambao ulikuwa ukioneshwa na marafiki zake na John na hata wafanyakazi wenzake sasa ukawa umefika ukingoni. Wakajitahidi sana kumvumilia nakumuona kama mgonjwa, ikawabidi waingilie kati ugomvi ule aliokuwa ameuanzisha John mule wodini.
“Hivi John rafiki yetu? uko sahihi kweli kwa unachokinena mbele ya mkeo. hivi unajua thamani yake wewe? Si mkeo wa ndoa huyu”
“Hata kama mke wa ndoa jamani lakini siwezi nikaponeshwa hiki kidonda ambacho kimenitokea cha kuondokewa na Angel?”
“Angel? Angel ndio nani?, Maana sisi kama wafanyakazi wenzako tunamtambua Janet kama mkeo na hata kwenye nyaraka zote za kwako za ofisini zinamtambua mkeo kama mrithi wa vitu vyako japokuwa bado huna mtoto”
Akili ya john sasa ikawa kama imeanza kuelewa kitu gani anachosemeshwa, japo alinyanyuka alijikuta mwenyewe akirudi tena mpaka chini kukaa kitandani huku akichukuwa mkono wake na kumshika mkewe Janet. Alimuangalia mkewe kwa jicho la aibu na kukaa kimya kwa muda kisha.
“Nakupenda sana Mke wangu!!”
“Nakupenda pia Mume wangu!”
Mwili wa Janet ulijihisi kusisimka, Akamwangalia rafiki yake Mary waliokuja naye kwa tabasamu. Akaifananisha siku hii kama ile siku yake ya ndoa walipokuwa wakifungishwa kanisani na mchungaji. Kitendo cha kuchukuwa chombo kingine na kumuwekea tena uji mumewe alifananisha na tukio la kuchukuwa pete na kumvalisha John. Moyo wa Janet haukuwa tayari kuvunjika haswa kwa mtu ambaye hata hamfahamu. Jina la Angel sasa likawa limemfutika John ghafla. Akajihisi kuwa na ganzi ya mwili kwa muda, kila akinyoosha shingo yake kuwaona wageni waliomtembelea ndipo na akili yake ikawa inafanya kazi vizuri.
“Haya kunywa basi mume wangu?”
“Sawa nipe taratibu tu”
John alikubali kupokea vijiko vya uji kutoka kwa mkewe Janet nakunywa. Hakuwa mbishi tena kama alivyokuwa hapo awali. Kila mmoja aliyekuja hapo kumtembelea alikuwa na sura ya tabasamu kuona John akiwa katika hali ya furaha na amani kwa mkewe. Alipomaliza kunywa uji tu, bosi wake aliyekuwepo pembeni akamkabidhi bahasha ya kaki iliyokuwa na kiasi kidogo cha pesa ndani yake kisha akamuaga. Muda wote Mary jirani yake na Janet alikuwa pembeni akimsubiria Janet waondoke lakini haikuwezekana kuongozana naye tena.
“Janet?, wacha na mimi niwahi nyumbani kupika si unajua sijaandaa chochote na watoto niliwaacha wameenda shule”
“Haya mimi acha niwe karibu na mgonjwa wangu, tutaonana huko huko nyumbani shosti”
“Haya baadaye, shemeji?”
“Naam!!
ENDELEA KUSOMA HAPA>>>>>>>>>>>
Post a Comment