HIVI NDIVYO MAN UTD ILIVYOUAWA OT JANA NA MAN CITY
https://menacotz.blogspot.com/2013/04/hivi-ndivyo-man-utd-ilivyouawa-ot-jana.html
MSHAMBULIAJI Sergio Kun Aguero
amewaumiza Manchester United na kuchelewesha sherehe zao Mashetani hao
Wekundu kushangilia taji la ubingwa.
Mkali huyo ambaye bao lake liliipa
ubingwa wa Ligi Kuu Manchester City msimu uliopita usiku huu ameifungia
timu hiyo bao la ushindi zikiwa zimesalia dakika 11 mchezo kwisha Uwanja
wa Old Trafford na kuipa ushindi mfululizo timu hiyo dhidi ya wapinzani
wao hao kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 41.
Kipigo hicho cha kwanza kwa United tangu
Novemba, pia kimemaliza rekodi yao ya kutofungwa ndani ya mechi 18 na
kupunguza idadi ya pointi zao za kuongoza kileleni mwa Ligi Kuu hadi
kubaki 12.
Mbaya wao: Sergio Aguero amewapa raha Manchester City leo kwa bao lake la ushindi
Anachomesha: Vincent Kompany (kushoto) akijifunga
Zikiwa zimesalia mechi saba tu Ligi Kuu kufikia tamati, bado United wana nafasi kubwa ya kutwaa uibingwa.
James Milner alitangulia kuifungia Man
City dakika ya 51, lakini Nahodha Vincent Kompany akajifunga
kuisawazishia United dakika ya 59 kabla ya Aguero kufunga la ushindi
dakika ya 78.
Katika mchezo huo, kikosi cha Manchester
United kilikuwa: De Gea, Rafael, Evra, Jones, Ferdinand, Giggs,
Carrick, Young/Kagawa dk90, Rooney/Hernandez dk85, Welbeck/Valencia dk80
na Van Persie
Manchester City: Hart, Zabaleta, Kompany, Clichy, Nastasic, Milner, Nasri/Aguero dk71, Barry, Silva/Lescott dk90, Y Toure na Tevez/Garcia dk90.
Mkwara: Gareth Barry (katikati) akimchimba mkwara Rio Ferdinand (kulia)
Mkwidano: Barry pia alikwidana na na kutupiana maneno Ryan Giggs (katikati)
Post a Comment