MBOWE NA ZITTO WAUNGURUMA TABORA

>> MBOWE ASEMA HAWATAMPOKEA KIONGOZI ALIYEFUKUZWA CCM


 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Bw.Freeman Mbowe akizungumza katika mkutano wa ndani wa chama hicho wakati wa uzinduzi wa kanda ya Magharibi uliofanyika mjini Tabora katika ukumbi wa Chuo cha ualimu TTC.
 
 Naibu katibu mkuu Chadema Bw.Zitto Kabwe ambaye pia alipata fursa ya kuzungumza katika mkutano huo wa ndani uliowakutanisha wajumbe kutoka mikoa ya Kigoma,Katavi na Tabora.
 Mwenyekiti wa Chadema Bw.Freeman Mbowe akipokelewa na baadhi ya viongozi wa wanachama wa Chadema mikoa ya kanda ya Magharibi.

Mwenyekiti wa Taifa  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,Bw.Freeman Mbowe amesema kamwe Chadema haitakuwa tayari kupokea na kuwapa nafasi  za uongozi viongozi watakaofukuzwa na CCM na kuja kutaka kujiunga na Chadema.

Bw.Mbowe ametoa kauli hiyo leo  hapa mjini Tabora kwenye ukumbi wa  Chuo cha ualimu katika mkutano wa  ndani wakati akizungumza na baadhi ya makamanda wa Chama hicho kanda ya magharibi inayojumuisha mikoa ya  Kigoma,Katavi na Tabora.

Alisema dhamira ya Chadema kwasasa ni kukiimarisha chama hicho na kupata viongozi walioandaliwa badala ya viongozi wanaozuka kama wanavyopatikana kwa vyama vingine vya kisiasa nchini huku akikitolea mfano Chama cha Mapinduzi ambacho idadi kubwa ya viongozi wake wanapatikana kutokana na uwezo wao wa kifedha akimaanisha wamekuwa watoaji wa rushwa hasa unapofikia wakati wa uchaguzi.

Mbowe akifafanua hilo mbele ya wajumbe hao alisema Chadema itahakikisha kiongozi kuanzia ngazi  ya  chini atakuwa na wajibu wa kuwatumikia wananchi na endapo atabainika kutowajibika katika kutekeleza majukumu yake hakitasita kuchukua hatua kwa mujibu wa katiba wa katiba ya chama hicho ikiwa ni pamoja na kumvua madaraka.

Aidha akizungumzia lengo la kuanzishwa kwa kanda hapa nchini,Mbowe alisema sababu kubwa na ya msingi ni kutaka kuwa na uwezo wa kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi jambo ambalo limekuwa ni gumu kwa Serikali inayoongozwa na chama cha mapinduzi.  

Hata hivyo Mwenyekiti huyo ambaye pia  ni kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni alisema lazima kwasasa wabunge wa Chadema watapimwa uwezo wao wa uongozi kutokana na utaratibu huu wa kanda na namna wanavyoweza kutekeleza majukumu yao kwa kusaidiana kati ya mbunge na mbunge ambao watakuwa katika kanda moja licha ya kuwa watakuwa wakitofautiana majimbo.

Kwaupande wake naibu katibu mkuu wa Chadema ngazi Taifa Bw.Zitto Kabwe aliwataka viongozi hao Chadema kanda ya magharibi kuwa tayari kujitolea kwa ajili ya Chama chao wakati huu wa kipindi kigumu alichodai kuwa ni wakati wa kuimarisha chama hicho kwa ngazi ya kanda mpango ambao ni mpya tangu kuanzishwa kwa Chadema miaka 22 iliyopita.

Related

SIASA 4538307741283183342

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item