SITAISAHAU facebook-------------21
https://menacotz.blogspot.com/2013/04/sitaisahau-facebook-21.html
MTUNZI: Emmy John P.
MAWASILIANO: 0654 960040
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
Sasa tukazidi kufunguka akili kuwa yule nyoka anawaona watu wenye alama. Na yawezekana ni nyoka huyu yupo katika kuwamiliki wanadamu kwa chapa yake ya hatari.
Swali kuu likabaki. Tunatoka vipi katika pori hilo.Mwanaume yule hakuzimia, alikuwa na timamu zake. Tukamweleza kwa kifupi naye akajieleza kuwa, tamaa ya utajiri imemtupia katika shimo hili baya.
Yule mwanaume alijitambulisha kwa jina la Samson alikumbuka vyema kuwa kabla ya kufika hapo alikuwa mkazi wa jijini Mwanza na alikuwa mwanafunzi katika chuo cha biashara (CBE) tawi dogo la jijini Mwanza.
Huyu alikuwa Samson kweli maana alikuwa ni mbabe sana. Lile kovu lake la kwenye paja halikumsumbua. Tulitembea kidogo akachuma majani fulani akayasagasaga akayaweka katika lile kovu. Hapa sasa aligumia kwa maumivu. Bila shaka ile dawa ilikuwa kali sana.
Akaniwekea na mimi katika kovu langu. Nikapiga mayowe. Akanikamata imara. Hadi maumivu yalipotulia kidogo. Jenipher hakutaka kovu lake la sikioni liguswe aliweza kuyakadiria maumivu makali ya dawa ile.
SASA ENDELEA KUSOMA HAPA>>>>>>>>>>>>>
Post a Comment