KAMA ULIKUWA HUJI HIZI NDIO SABABU ZILIZOWAFUKUZA VIGOGO WA BANDARI HAPA


Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Ephraim Mgawe.
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amewatimua kazi vigogo watano wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu na kuisababishia Serikali hasara kubwa.

Waliotimuliwa ni aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Ephraim Mgawe, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Huduma, Hamadi Koshuma, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Miundombinu, Julius Mfuko, Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Cassian Ngamilo, Meneja Kituo cha Kupakulia Mafuta, Tumaini Massaro.

Akitangaza uamuzi huo jana mbele ya waandishi wa habari, Dk Mwakyembe alitaja tuhuma za kila mmoja ambazo zilisababisha uamuzi huo kuchukuliwa.

Akiainisha tuhuma zilizomfukuzisha kazi Mgawe kuanzia Ijumaa iliyopita Januari 18, Dk Mwakyembe alisema ni pamoja na uzembe uliokithiri.audifacejackson.blogspot.com

Dk Mwakyembe alidai kuwa Mgawe alizembea na kuruhusu kuwapo kwa muda mrefu utaratibu usiofaa wa upokeaji na uondoshwaji bandarini wa mafuta machafu.

Katika tuhuma hiyo, Mgawe anadaiwa kuachia kiasi kikubwa cha mafuta safi kuibwa; na kushindwa kudhibiti kiwango cha utoaji bandarini wa mafuta machafu kinyume na mikataba iliyopo.


Tuhuma ya pili iliyomwondoa Mgawe, ni ufanisi duni ambao Dk Mwakyembe alifafanua kuwa alishindwa kudhibiti wizi uliokithiri bandarini wa mizigo na mali ya Mamlaka.

Pia anadaiwa kushindwa kusimamia utekelezaji wa mkataba kati ya Kitengo cha Kuhudumia Kontena Bandarini (TICTS) na TPA ambapo TICTS kwa muda mrefu inadaiwa imekuwa ikikiuka mkataba huo.

Pia Mgawe anadaiwa kuipotosha Bodi hata ikaridhia uanzishwaji wa chombo cha pili cha ununuzi ndani ya Mamlaka kinyume cha sheria.

Mgawe pia inadaiwa alikosa uaminifu pindukia, ambapo anadaiwa kutumia chombo cha pili cha ununuzi kilichoanzishwa kinyume cha sheria na kuingia zabuni bila kufuata utaratibu na kanuni za zabuni kama zilivyoainishwa na Sheria ya Ununuzi.

Pia inadaiwa miradi mingi iliyongiwa kwa njia hiyo ya chombo cha pili cha ununuzi, haikuwa na tija kwa Mamlaka zaidi ya matumizi mabaya ya fedha za umma.audifacejackson.blogspot.com

Kwa mujibu wa Dk Mwakyembe, pia alikiuka sheria na utaratibu ambapo anadaiwa kuingia mkataba na Kampuni ya China Communications Construction Ltd (CCCC) bila kuishirikisha Bodi ya Zabuni ya Mamlaka.
Pia anadaiwa kuongeza mishahara kwa asilimia 15 Julai mosi mwaka jana bila idhini ya Waziri wa Uchukuzi, hivyo kukiuka utaratibu uliowekwa na sheria.

Tuhuma zilizomng’oa Koshuma kwa mujibu wa Dk Mwakyembe ni nne; ya matumizi mabaya ya madaraka. Katika hilo, Naibu Mkurugenzi Mkuu huyo wa Huduma, anadaiwa kuruhusu michakato ya zabuni bila kufuata utaratibu kwa kisingizio cha miradi mikubwa.

Koshuma pia anadaiwa kuwa na ufanisi duni, ambapo akiwa Mjumbe wa Bodi ya Zabuni, alishindwa kuijulisha Bodi ya Mamlaka ya Ununuzi ya Umma (PPRA), kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya Ununuzi.

Ukiukwaji huo ulifafanuliwa kuwa ni wa kuruhusu Mamlaka kuingia mkataba wa kibiashara na CCCC bila kushirikisha Bodi ya Zabuni na kushindwa kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka katika udhibiti na uendeshaji.

Pia amekosa uaminifu kupindukia, ambapo anadaiwa kushiriki kuipotosha Bodi hata kuanzishwa chombo cha pili cha ununuzi kinyume cha sheria.
audifacejackson.blogspot.com
Alidaiwa kutumia chombo hicho batili bila kufuata utaratibu kwa kisingizio cha miradi mikubwa ambapo mingi iliyoingiwa kwa njia hiyo, haikuwa na tija kwa Mamlaka zaidi ya matumizi mabaya ya fedha za umma.
Koshuma anadaiwa kukiuka sheria na taratibu kwa kushiriki kuingia mkataba na CCCC bila kushirikisha Bodi ya Zabuni ya Mamlaka.

Pia anadaiwa kushiriki uamuzi wa kuongeza mishahara kwa asilimia 15 kuanzia Julai mosi, mwaka jana bila idhini ya Waziri wa Uchukuzi.audifacejackson.blogspot.com

Kwa upande wa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Miundombinu, Mfuko, Dk Mwakyembe alisema alishindwa kusimamia maandalizi ya miradi ya miundombinu ya Mamlaka.

Kwa mfano miradi ya ex-AMI yard, Port Community System na CCTV kwa muda mrefu iko kwenye utekelezaji bila kukamilika kutokana na misingi mibovu ya maandalizi. Ilielezwa kuwa fedha nyingi za Mamlaka zilitumika kwenye miradi hiyo bila matokeo tarajiwa.

Pia alishindwa kusimamia utekelezaji wa mikataba na kusababisha kutokamilika kwa wakati na kusababishia Mamlaka hasara kubwa.

Mfuko alishindwa kuisimamia kwa ufanisi divisheni ya maendeleo ya miundombinu na kuathiri maendeleo ya Mamlaka kwa ujumla.

Pia alishindwa kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka katika udhibiti na uendeshaji wa Mamlaka.

Mbali na wakurugenzi hao, Dk Mwakyembe pia alitimua mameneja akiwamo Ngamilo ambaye inadaiwa alitumia madaraka vibaya, uzembe uliokithiri na kushindwa kusimamia mkataba wa mafuta machafu.

Pia alidaiwa kushindwa kusimamia ulinzi wa mali za wateja, kutoa nyongeza ya mkataba kinyume cha sheria.

Naye Meneja wa Kitengo cha Mafuta (KOJ), Tumaini ameachishwa kazi kutokana na madai ya uzembe uliokithiri, kushindwa kusimamia udhibiti wa mafuta machafu na kusababishia Serikali hasara kubwa pamoja na ufanisi duni.

Hata hivyo, Dk Mwakyembe alisema wataendelea kusimamia bandari ipasavyo, kwa kuwa ni chombo muhimu sana hivyo michezo kama hiyo ikiendelezwa, nchi haitaondokana na umasikini na mfumuko wa bei.

Alisema kuachishwa kazi kwa watu hao ni hatua za awali, na Bodi inaendelea na kazi yake, kwa hatua zaidi ikiwa ni pamoja na kufahamu ni hasara kiasi gani imesababishwa na uzembe huo.

Related

TPA 2308943001343181436

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item