AFCON: Ethiopia yaivuruga Zambia,Nigeria yabanwa

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Zambia (Chipolopolo) Christopher Katongo (kulia) akijaribu kumtoka beki wa timu ya Taifa ya Ethiopia                Afrika Kusini
MABIGWA watetezi wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) Zambia Chipolopolo imeshindwa kuonyesha umwamba wao mbele ya wageni wa fainali hizo timu ya Ethiopia ambayo ndiyo wawakilishi pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Chipolopolo imelazishwa sare ya kufungana bao 1-1, katika mechi hiyo Zambia ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza iliyofungwa na Collins Mbesuma dakika 45 kabla ya Ethiopia kusawazisha bao hilo kupitia kwa nahodha wake Adane Girma dakika 64.
Mchezo wa pili kati ya Nigeria na Bukinafaso pia imemalizika kwa sare ya kufunga bao 1-1, Nigeria ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza ikifungwa na E Emenike dakika ya (22) hata Nigeria walinyang'anywa tonge mdomoni baada ya Bukinafaso kusawazisha bao hilo dakika ya 90 kupitia kwa A Traore matokeo hayo yamezidi kuiweka Zambia katika mazingira magumu ya kutetea ubingwa wake kupitia kundi hilo la C.
Kesho kuna mechi ya kali yenye ushindano mkubwa kati ya Ivory Coast na Togo ikifuatiwa na mechi kati ya  Tunisia na Algeria katika Uwanja wa  Royal Bafokeng.

Related

AFCON 9099010724064686591

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item