THIAGO ALCANTARA NJIANI KUJIUNGA NA MACHESTER UNITED

Thiago 22, yuko katika hatua za mwisho za kujiunga na club ya Manchester United. Kiungo huyo mkabaji amekuwa akitolewa macho na timu hiyo ya Uingereza toka mwaka 2011 lakini ilikuwa ngumu kumng'oa Nou Camp.
Man Utd wameweza kumng'oa pale baada ya mchezaji huyo kuomba kuondoka Nou Camp. Thiago ameomba kuondoka kwasababu anahitaji kupata namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza ili aweze kuitwa kuichezea timu ya taifa ya Hispnia kwenye kombe la dunia mwaka kule Brazil.
Hata hivyo Thiago ataweza kupata namba ya kudumu pale OT kwasababu Ni Carrick pekee ambaye amekuwa akicheza nafas hiyo. Hivyo uwepo wake pale OT atakuwa na nafasi nzuri ya kuonesha kipaji chake kwenye michuano mbalimbali.
Alcantara ambaye ni captain wa Hispania U-21 iliyotwaa ubingwa wa Euro Championship pale Brazil alikaribishwa na mchezaji na rafiki yake David  De Gea mara baada ya ya kupiga hat-trick kwenye final. De Gea aliandika kwenye mpira wake kuwa "tukutane Manchester United " hiyo ilikuwa ni Ishara tosha kuwa Thiago yuko njiani kuelekea OT.
Kwa mujibu wa habari mbalimbali kwenye magazeti ya Ulaya, ni kwamba Thiago ataenda OT kwa ada ya £17 million huku akililpwa £5 million kwa mwaka.

Related

USAJILI 2224434513495386923

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item