WALIMU WALALA JIKONI -IGUNGA

Walimu walala jikoni kwa
miaka mitatu!
KATIKA hali ya kusikitisha, walimu
wa Shule ya
Msingi Iyogelo iliyoko katika kata ya
Kining’inila Wilaya ya Igunga
mkoani Tabora,
wamekuwa wakiishi jikoni kwa zaidi
ya miaka
mitatu, kutokana na ukosefu wa
nyumba za
walimu katika shule hiyo. walimu
hao Paul Kennedy na Elia
Nzowa, walisema wamekuwa
wakikumbana na
adha hiyo kwa zaidi ya miaka
mitatu.
Walimu hao, walisema kutokana na
hali hiyo,
wamekuwa wakipata shida nyakati
za usiku, kwa
kuwa jiko hilo ni dogo na halina
hewa ya
kutosha.
“Sisi walimu tunaishi katika
mazingira magumu,
kwa sababu tunaipenda kazi yetu
ndio maana
tunaendelea kuishi hapa kwa
uvumilivu,”
alisema.
Kutokana na hali hiyo, wameiomba
Serikali
kuwajengea mazingira mazuri ya
kuishi na
kuboresha nyumba za walimu
shuleni hapo, ili
kuinua kiwango cha elimu katika
shule hiyo na
taifa kwa ujumla.
Nao wananchi wa kata ya
Kining’inila, walisema
suala la walimu kuishi jikoni
wanalitambua,
lakini kutokana na kukabiliwa na
ukosefu wa
chakula, wameshindwa kuchangia
michango
kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za
walimu
shuleni hapo.
Naye, Kaimu Ofisa Mtendaji wa
Kata ya
Kining’inila, Abel Isaka alikiri
kuwepo kwa
ukosefu wa nyumba za walimu
shuleni hapo na
kusema kuwa suala la ukosefu wa
chakula
katika kata hiyo, ndilo lililochangia
wananchi
kushindwa kuchangia fedha kwa
ajili ya ujenzi
wa nyumba za walimu.
Kwa upande wake, Ofisa Elimu
Shule za Msingi
Wilaya ya Igunga, Juma Selemani
alithibitisha
kuwepo kwa tatizo hilo

Habari hii kwa hisani ya NASSOR WAZZAMBI

Related

MATUKIO 639808560517088863

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item