UCHAGUZI WA NDANI YA CHADEMA KUNA NINI? : NAULIZA TU
Nauliza tu jamani!
1. Hivi uchaguzi wa Ndani wa Chama kinachojieleza mbele ya umma kuwa kinajali Demokrasia na Maendeleo umeshafanyika? Kama ndio nani aliibuka Mshindi kwenye Kinyang'anyiro cha Uenyekiti ngazi ya Taifa? Je BAVICHA nani kamtoa Heche hiyo nafasi? na Kama Bado Denokrasia iko wapi au katiba ina ruhusu kukaa madarakani kwa muda gani? Je demokrasia ya ukweli ni ipi kuongoza kibabe au kwa ridhaa ya wanachama? Kama wanaamini katika Demokrasia, Je kwanini bado wapo madarakani, Au wanaogopa kuziachia hizo nafasi na watu waliowaweka kwenye nafasi za uongozi kuwa zitachukuliwa na watu wengine? Wamekuwa wakikosoa sana Uchaguzi wa ndani wa CCM kuwa umejaa RUSHWA, na Upendeleo kwa watoto wa vigogo, Sasa Nilitegemea mwaka huu Chama kinachohubiri Demokrasia kwa kufanya uchaguzi wa ndani usio na Rushwa na Upendeleo, sasa NAULIZA JE UCHAGUZI WA NDANI KUNA NINI?
Post a Comment