WENJE NDANI YA KASHFA NZITO YA UFISADI WA MAMILIONI YA FEDHA YA MIRADI YA JIJI LA MWANZA.
TAARIFA KWA UMMA WA WANA
MWANZA,WATANZANIA NA VYOMBO VYA USIMAMIZI WA SHERIA JUU YA UFISADI WA
KUTISHA NA UBADHILIFU WA FEDHA ZA UMMA KATIKA MIRADI YA UJENZI WA JENGO LA KLINIKI
YA MAMA NA MTOTO UTEMINI NA UJENZI WA OFISI NA STOO ZA MADAWA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA.
Kwanza nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda na kunipa afya,maana afya yangu ni njema kuliko kipindi chotechote
kilichopata kuwako chini ya jua. niwashukuru wananchi wangu wanaoniombea katika kipindi
hiki kigumu cha kuitafuta haki yangu naya wananchi wangu wa Igoma. walionichagua bila kujali itikadi zao za kidini ,vyama vyao vya siasa ,pia wote wanaoniombea katika kipindi hiki kigumu cha mapito mazito, ni imani yangu
mapito haya ni tanuru linalonipika kuelekea ukamilifu wa kweli maana ili dhahabu iwe safi ni
lazima ipite katika kalibuni (tanuru) kisha hutoka ikiwa safi. Taarifa yangu ni kuhusiana na
mchakato wa ujenzi wa kituo cha Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto utemini iliyogubikwa na UFISADI wa kutisha huku wanaohusika wakijivika utakatifu bandia,na KUWALISHA WANANCHI UONGO MTAMU NA UKWELI BANDIA huku
wakijitanabaisha kwa wananchi kuwa wao ni watakatifu na watu makini kumbe kinyume chake ni jawabu.
Halmashauri ya jiji la Mwanza ilipokea fedha kiasi cha shillingi bilioni tatu nukta moja (3.1)
kutoka Benki Kuu ya Tanzania,kama fidia kwa ajili ya eneo la kiwanja cha MAKONGORO KLINIKI
cha halmashauri ya jiji la MWANZA ,kilipo kituo cha Makongoro Kliniki ili kufidia kliniki ya mama na mtoto,hivyo halmashauri iliazimia kujenga kituo kingine jirani na shule ya msingi Mirongo maeneo ya utemini na kujenga jengo la ofisi kwa ajili ya watumishi idara ya afya, Mkurugenzi wa jiji la Mwanza na ofisi za meya wa jiji la
Mwanza ,jengo hilo la ofisi limejengwa nyuma ya jengo la sasa la halmashauri ya jiji la Mwanza. kiwanja hicho kilichukuliwa na Benki hiyo KWA AJILI YA SHUGHULI ZAKE ZA KIBENKI. Jengo la kliniki ya mama na mtoto lina ukubwa wa mita za mraba 906 likiwa jirani na shule ya msingi ya Mirongo. Jengo ni maalumu kwa ajili ya mama na
mtoto litakuwa na idara zifuatazo:- uzazi wa
mpango, Afya ya mtoto (PAEDIATRIC), C.T.C, PMTCT, kuharisha, chanjo, madawa na sehemu nyingine kama jiko sehemu ya kufulia na ofisi za
utawala. Washauri wa mradi huu ni kama wafuatao;
1. Msanifu majengo: K & M Archplan(T) P.O.BOX
32025 DSM
2. Structural Engineers: S & F Consultants Ltd
P.O.BOX 13763 DSM
3. Senices Engineers: Electic(T) Ltd P.O.BOX
23437 DSM
4. Quantity surveyor: Cost Data consult Ltd
P.O.BOX 33897 DSM
5. Mkandarasi: M/S JASCIE & CO. Ltd P.O.BOX
2962 DSM
Baada ya taratibu zote za manunuzi kukamilika mkandarasi M/S JASCIE @CO. LTD alipatikana na kufunga mkataba MCC/089/2011/2012/W/07 na
Halmashauri wenye jumla ya fedha
853,568,493.42.00 na ulipangwa kuanza tarehe 1st March 2012 na kukamilika tarehe 07th March 2013. Wasimamizi wa maslahi ya wananchi wameungana na watendaji kutafuna maslahi
wanamwanza ,mikataba ya ujenzi wa miradi hiyo ilisainiwa na aliyekuwa meya wa jiji la mwanza
Josephat Kanyonyi Manyerere ambaye cha kushangaza ni kwamba jengo hilo lilisainiwa kujengwa kwa gharama ya shillingI za kitanzania 853,568,493.42.00 na ulipangwa kuanzia tarehe 1 march, 2012 na ukamilike tarehe 7march2013 na mkandarasi ni JASCE 8 C0 LTD mkataba MCC/089/2011/2011/2012/W/07 cha kushangaza mkandarasi mpaka sasa amelipa fedha nyingi zaidi ya zile zilizo kwenye mkataba
kiasi cha shilingi 1,101,453,752.68 na cha kushangaza ujenzi huo umetumia fedha zaidi nabado hakuna jengo la choo na incinerator (sehemu ya kuchomea takataka) Maswali yanayoulizwa hapa ni kwamba nani ? aliongeza kiasi cha ziada cha fedha hadi kufikia billion 1.1 nje na makubaliano katika mkataba tajwa.
Taarifa za kuamini baada ya kung’olewa meya Manyerere aliyekuwa ofisini kama meya na Naibu meya Charles Chinchibera kushirikiana na watendaji wa halmashauri Chinchibera alisaini nyongeza ya fedha shilingi 247,885,259 nje ya mkataba na kufanya kiasi cha fedha nje ya mkataba katika kliniki ya mama na watoto utemini lakini jengo hilo bado halina choo,uzio,sakafu yanje ya uzio,sehemu ya kuchomea takataka na inahitajika kiasi cha 270,000,000 shilingi milioni mia mbili na sabini tena ili jengo liweze kukamilika ,hawa wawakilishi wa wananchi wameungana na watendaji kutafuna keki ya wana mwanza bila huruma.
Ezekiah Wenje ni mwanamkakati mwingine katika kadhia hii,kutokana na sababu zifuatazo; katika harakati za kusema na kueleza mwenendo usioridhisha wa meya wa jiji Manyerere(wakati huo) alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha Manyerere haguswi na kumlinda kama mboni ya jicho,Wenje alisimama kidete ili kuhakikisha Manyerere haguswi wala kubughuziwa,ili kulinda
maslahi yao,Wenje hataki kuzungumzia mpango mzima kuhusiana na mwenendo wa ujenzi wa jengo hili amekuwa ni mtu wa kutoa vimemo,vikaoni ili wengine wazungumzie suala la jengo hili,huku yeye akijiweka pembeni kama siyo mwakilishi na msimamizi wa maslahi ya wanamwanza Wakati sisi tulipokuwa tukilalamikia utendaji dhaifu na usioridhisha wa ndugu Manyerere usioendana kasi na matarajio ya wananchi yeye alikuwa mstari wa mbele kumkingia kifua na kujenga aminisho la kustiri mivumo ya kuwa wao ni makamanda wa ukweli kumbe ni mafarisayo wanaoyapaka rangi makaburi nje wakati ndani yamejaa mifupa.
Ndugu Wenje tangu Manyerere alipoondolewa kitini na uchaguzi mpya wa meya kufanyika katika halmashauri mbili ilemela na jiji la Mwanza yeye kama mjumbe wa kamati ya fedha na uongozi ya halmashauri ya jiji la Mwanza hajawahi kuhudhuria kikao yapata miezi kumi kwa kisingizio ya kuwa yuko Bungeni na kwenye vikao vya kamati lakini anachukua posho za vikao bila kuhudhuria na ushahidi upo mweupe kabisa anaogopa kusutwa na ukweli
kudhihirika ,amejiweka pembeni na kuwa mtu matamko na mikutano isiyo na tija kwa lengo la kujiweka mbali ili aje akache lawama kuwa yeye si mhusika katika hujuma za fedha za miradi ya majengo haya.Hadi sasa mkandarasi amekwisha kulipwa jumla ya shilingi 1,101,453,752.68.
wakati haki yake ni 853,568,493.42.00kumbe wakati sisi tunaijenga taswira ya mwanza na chama wao walijenga mambo yao. Na kuchochea chuki kwa umma kuwa sisi tunavuruga chama kumbe nyuma ya pazia wana ajenda yao hatimaye leo imethibitika huko tuendako tutaona mengi. ujenzi wa jengo la ofisi kwa ajili ya watumishi wa idara ya afya nyuma ya ofisi za sasa za halmashauri,lenye kiwango cha ghorofa moja lenye ukubwa wa mita za miraba 3,345 nyuma ya ofisi za halmashauri ya jiji la mwanza limegubikwa na utata mkubwa sana linaloacha maswali yasiyojibika mpaka sasa chini ya mkandarasi M/S Tanzania Builiding Works P.o
Box 2962 Dar es salaam mkataba wa ujenzi wa jengo hili la ofisi na stoo za madawa ni
MCC/089/2011/2012/W/08 ambao ulianza March 5/2012 na ulipangwa ukamilike 17/ agosti/2013 kwa gharama ya shilingi 2,108,197,292.50 bilion mbili mia moja na nane milioni mia moja tisini na saba elfu mia mbili tisini na mbili na senti hamsini ikiwa ni pamoja na VAT.Washauri na wasimamizi wa kazi walikuwa kama ilivyooneshwa hapa chini;
1. Msanifu Majengo: K&M Archplan(T)P.O.BOX
32625 DSM
2. Structural Engineers: S&F Consultant Ltd
P.O.BOX 13763 DSM
3. Services Engineers: Electric(T)Ltd P.O.Box
23437 DSM
4. Quantity Survryor: Cost Data Consult Ltd P.O.
BOX 33897
5. Mkandarasi : Tanzania Building Works P.O
BOX 2962 DSM(Class 1)
Lakini cha kushangaza kuna vitu ambavyo vina shangaza zaidi gharama za ujenzi wa mradi huu
ni kubwa kulinganisha na jengo linalojengwa hivyo kushangaza na kuhuzunisha wana mwanza
maana mikataba ya ujenzi wa majengo haya yote ilisaini na aliyekuwa meya wa jiji la Mwanza
wakati ho ndugu JOSEPHAT MANYERERE,na nyongeza ya pesa kinyume na mkataba ilifanyika
wakati Charles Chinchibera (aliyekuwa naibu meya)wakati huo akishikilia ofisi baada ya Manyerere kuondolewa kitini,waliongeza nyongeza ya mkataba wakishirikiana na baadhi
ya watumishi wa halmashauri ya jiji walifanya ubadhirifi huo mkubwa.
Mhusika mwingine ni Engineer Koyoya Fuko ambaye alikuwa ni mhandisi wa barabara huyu
ndiye aliyekuwa(MENEJA MRADI) msimamizi wa mradi kabla ya kuhamia halmashauri ya jiji la DSM yeye ndiye aliyekuwa jicho la halmashauri ya jiji la Mwanza,lakini cha kusikitisha walishirikiana na viongozi niliyowataja kimakusudi kuhujumu utekelezaji wa miradi hii muhimu kwa wana mwanza na watanzania kwa ujumla, Fuko ni mhandisi wa barabara lakini cha kusikitisha yeye ndiye mtekelezaji wa miradi hii tata ambayo ina ufisadi ndani yake na unahujumu maslahi ya wananchi wa jiji la Mwanza, hadi sasa taarifa kamili pamoja na kukabidhi ofisi na kuhamia jiji la Dar es salaam ,hakuna taarifa alizokabidhi ofisi ya uhandisi ikielezea kwa kina mpaka pale kikao cha kamati ya fedha na uongozi chini ya meya wa sasa kuomba taarifa ya utekelezeji wa miradi hiyo yote.
Wahusika wakuu na wanamikakati wa mpango
mzima ni:-
1. Ezekia Dibongo Wenje (mbunge wa jimbo la
Nyamagana)
2. Josephat Manyerere (aliyekuwa meya wa jiji la
Mwanza)
3. Charles Marwa Chinchibera (aliyekuwa naibu
meya wa jiji la Mwanza)
4. Koyoya Fuko (Engineer wa Barabara)
• Taratibu za manunuzi zimekiukwa
• Mikataba imevunjwa
• Baadhi ya nyaraka zimenyofolewa ili kufichwa ukweli
• Wasimamizi wa maslahi ya wananchi kushirikiana na watendaji wa halmashauri
kufanya ufisadi huo na hujuma kwa wananchi
• Taarifa ya fedha taslimu hazipo maana ujenzi wa majengo hayo haukutegemea makusanyo yetu
ya ndani au ruzuku serikalini pesa ilikuwepo taslimu lakini miradi imesimama
Mambo ya kuzingatia
1. Taratibu za manunuzi ziangaliwe upya
2. Mikataba ipitiwe upya
3. Wahusika wachukuliwe hatua
4. Gharama za ujenzi haziendani na uhalisia wa thamani ya soko
5. Uthamani wa kazi iliyofanyika ufanyike ili kubaini gharama halisi iliyotumika
6. Fedha za miradi hiyo imekwenda wapi maana
miradi hiyo imesimama.
amini nawambia jiwe walilolikataa waashi limegeuka kuwa jiwe kuu la pembeni yeyote atakaye anguka juu yake atavunjika vunjika na
litae muangukia litamsaga tikitiki.
CHAGULANI ADAMS IBRAHIM [ MAJI ]
Post a Comment