UNANIDANGANYA WENGER :- JOEL CHUKU VERMINATOR

Mti Bila Mzizi Utakua Vipi Miaka Nane Bila Kombe Na vile Tulivyokua Tunajiongopea
Wenyewe Kila Siku...... Tulikua na Tony Adams wetu, Martin Keawon
wetu na Ray Palour wetu... Mwisho mwisho tukawa na Sol Campbell wetu akatutumikia mpaka pale tulipo amua wenyewe kumwambia
sasa basi nenda sehemu nyingine....
Walikua na Gerrard wao na pacha wake Carragher wale wengine wakawa na Giggs wao na ndugu zake walio grew up together Scholes na Gary Neville na mdogo wao Rio Ferdinand ....Kule darajani kuna kiongozi na msaidizi wake nikimaanisha Captain John Terry na msaidizi wake Super Frank Lampard..

Hata ukienda Barcelona kule kuna Puyol na mzee mwenzake Xavi Hernandez na wale Madridista wakawa na Raul Wao na kipa wake
Casillas...

Ac Millan walikua na watu wao Paul Maldini na pacha wake Alessandro Nesta, na muhuni
Gattuso na Pirlo wamewatumia hadi walipochoka wenyewe...

Wajeruman Bavarians wana Philip Lahm wao pamoja Bastian Shwanstiger wake sasa hivi wana
mdogo wao Thomas Muller...

Ni kwamba hamna team itakayofanikiwa pasipo kua na mizizi imara na hiyo mizizi imara ya team haitengenezwi kutokana na kujaza wachezaji wengi wa kigeni ndani ya team Bali
inatengenezwa na wachezaji wazawa walio komaa na wenye viwango bora kabisa vya dunia alafu sasa team nzima inajengwa ikiwazunguka wachezaji hawa wazalendo... Kitu ambacho Arsene Wenger alikisahau pale kizazi chetu cha wazawa kilivyokua kinazeeka pasipo kutafuta kizazi kingine kipya kilichokua tayari kwa muda ule kuleta matunda alisahau kila team ina hitaji mizizi ili kufanya vizuri, hata haya maneno tunayotumia ili yatamkwe vizuri
yalete maana Yana mizizi yake...
Hawa superstars wachezaji wakigeni hua sio watu wa kuaminika wengi wao wanacheza kwa kuangalia career zao zimekaa vipi mtu kasafiri kutoka kwenye nchi ya utamaduni mwingine kuja
kutafuta maisha kaacha familia na ukoo wake huko atokako anachojua ni kufanya kile kilicho
mleta tu, ingawa wapo wanao kua loyal ila ni wachache ni kama vile idadi ya wachezaji wakubwa wazawa wanaondoka kwenye timu
kubwa za nchi zao ni wachache mno , na wengi wao wanasepa kwa matatizo binafsi na makocha
wao... Bila Beckham kugombna na Ferguson leo hii angestaafu akiwa united na best friend wake
Gary Neville ..ila huyu Erick Cantona alisema msinizingue
akawaachia united yao akasepa zake huku mpira ukiwa haujamuisha miguuni, van persie msimu wake mmoja alifanya vizuri akaenda kuchukua taji sehemu nyingine, Cristiano Ronaldo
alivyoona ameshinda kila kitu na United yake hakuona Sababu ya kubaki ... tena Luis Figo
akiwa ana shadadia kabisa Ronaldo aondoke united akaamua kumsikiliza mreno mwenzake na
kuondoka zake akiwaachia akina giggs Manchester yao walioshinda nayo mataji mengi zaid ya alioshinda Ronaldo na team iyo..

Fernando Torres wala hakufikiria mara mbili nyimbo alizokua akiimbiwa pale Anified alihitaji
kushinda champions league na Premier league akawaacha wenzake na kusababisha Gerrard
adondoshe chozi huku Gerrard mwenyewe ana amini anaweza kushinda taji hilo la ligi kuu akiwa
na Liverpool yake..... Thierry Henry alikua anafahamu kua yeye ni mungu mtu pale Arsenal ila hilo alimkuzuia kwenda Barcelona kutafuta champions league... Na Barcelona hawatakuja
kusahau usaliti waliofanyiwa na Luis Figo alipoamua kugeukia upande wa pili wa shilingi
na kujiunga na Real Madrid..

Hata Luis Suarez suala la kujiunga na Arsenal wala halikua gumu kwake kama Liverpool wasingebana alikua anaondoka, huyu ozil kwa ujeuri wake na kujiona yeye bora hakuona kama
kuna sababu ya kugombania namba kwakua hana kitu chochote cha kuprove, kama uwezo wake
tayari ameshaonesha akawaachia team yao akasepa, akina Ramos wanalalamika ila hata haijasaidia na hata arsenal msishangae siku
tukimzingua atataka kusepa..
Wakati wenzetu wakina giggs wao wanaanza kuzeeka wanaacha team mikononi mwa Rooney
na Carick wake ambao nao wakipotea Clevery na madogo wenzake watakua tayari .... Kule
Catalunya walijua haitachukua muda Xavi na puyol wake watachoka wakamrudisha cesc
fabregas nyumbani, kuna pique na Pedro wakiongozwa na kaka wao iniesta watakao Simama hadi pale wakina Batra na wenzake
watakapokua tayari....

Raul anaondoka Sergio Ramos anakomaa, Wakati casilas akiwa anachoka Morata Anaibuka kuja
kuungana na kaka yake Sergio Ramos kuiongoza Madrid yao.... Wakati Philip Lahm na Bastian
Shwanstiger wake wakiwa washafika kwenye kilele cha career zao, miaka michache ijayo wataanza safari ya kushuka chini wataiacha iyo team kwenye mikono salama ya goalkeeper
Neure , pamoja na wenzake badstuber, boateng, muller na mdogo wao Gotze wakina lahm
wataiacha team salama kama wao walivyoachiwa na akina Oliver Khani na wenzake..

Baada ya zama za del piero na bufon wake kuisha sasa hivi kuna chielini na Giovinco wake, naona na Ac Milan wanaijenga team yao upya ikiwazunguka el shaaraw na balotel wake...
Hapa ndio utagundua ni kiasi gani arsene Wenger aliniongopea mimi na Wewe na pia alijiongopea yeye mwenyewe, maana ilikua inafikia kipindi arsenal inacheza pasipo mchezaji wa kiingereza ndani ya kikosi na kama akiwepo basi ni Theo Walcott aliekua kitoto kidogo
kisicho na mbele wala nyuma.... Am not sure kama Arsene Wenger baada ya kusalitiwa na Ashley Cole aliamua kususa kwa waingereza au
labda ni kweli alikua anajiongopea yeye mwenyewe kwa kuwategemea zaidi superstars wa kigeni waliokuja kumkimbia na kufata mshahara mikubwa na mataji ...
Namalizia kwa kusema Team bila wachezaji wazawa walio loyal na wenye viwango bora basi haiwezi kua na mafanikio kamwe, Maybe Arsenal inaweza kushinda taji msimu huu ila ni kwakua tuna morale na hasira ya kushinda taji... ila kwa Arsenal kua real threat kwa team zingine na ku-maintain winning ways ni hadi hawa waingereza wetu wakomae wawe kati ya wachezaji walio na
ubora wa kiwango cha dunia..
Maybe kuanzia msimu unaofata ndio tutaanza kua real threat kwakua tutakua tunawachezaji
bora ambao hawafikirii maisha mengine nje ya arsenal yao kama alivyokua Tony Adams....
Na pia baada ya hapo tunatakiwa tuwe na balance nzuri kati kizazi kimoja hadi kingine cha wazawa Wakati wengine wakiwa wana zeeka basi wengine wawe tayari washakomaa kuendeleza
mapambano.

HUYU NI MDAU WA BLOG: JOEL CHUKU VERMINATOR WA GROUP MAARUFU LA MICHEZO KWENYE FACEBOOK, SPORTS XTRA CLOUDS FM.

Related

Sports 6779318111396063289

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item