HAPPY BIRTHDAY DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Ni jambo la kumshukuru Mungu pale unapotimiza miaka kazaa tangu ulipozaliwa, Unapoikumbuka siku hii naamini unakumbuka mengi yaliyotokea ndani ya maisha yako, mengine mazuri mengine ni mabaya, mengine ya furahisha na kutia moyo na mengine yanahuzunisha na kukatisha tamaa,

Pamoja na mambo yaliyotokea ndani ya maisha yako lakini bado umesimama na kupiginia kiti chako, na taifa lako. Unaongoza kwenye kipindi kigumu, yaani kipindi cha watu ulio wapi chakula wewe mwenyewe na waliposhiba  wakaanza kukutusi tena, Na maanisha ya kuwa umetupa elimu wewe mwenyewe lakini bado tuna kutusi wewe. Ila kwa kuwa wewe ni mzazi mwema na mvumilivu bado umetusamehe na unaendelea kujenga nchi.

Mh. Rais, wewe ni miongoni mwa watu wachache duniani wenye ustahimilifu na uvumilivu sana. Umejaribiwa kwa kila namna ili nchi yako isitawalike ila bado ulishinda na unaendelea kushinda, walianza na majambazi, wakaja Richmond, wakawa walimu, wakaja madoctor, yakafika maandamano, wakaja na gia ya katiba, wakaja kwenye uchaguzi wa chama, kina Banda, Kagame na Kenyatta, wakaja wa tindikali, wakuchoma makanisa, wang'oa kucha na meno na sasa wapo na Muswada. Lakini vyote hivyo na ambavyo sikuvitaja, umevipangua na bado nchi ina amani tunazidi kusonga. KWELI SI RAHISI KUWA RAIS,hasa taifa kama ambao vijana wanafundishwa kulalamika kuliko kufanya kazi.

Mwisho kabisa, napenda kukuombea kwa Mungu aendelee kukupa busara na hekima katika kutekeleza matakwa ya wananchi.

HUTAPENDWA NA KILA MTU, ILA MIMI NAKUPENDA.

Related

JK 3063133373812055210

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item