VIONGOZI, WANACHAMA NA WAFUASI WA CHADEMA NI WOGA.

Nawasalimu wote.

Napenda kumshukuru Mungu wa mbiguni kwa Rehema zake na kunifanya hai mpaka leo. Ama baada ya shukrani zangu naomba kueleza machache juu ya mambo machache yanayoendelea ndani ya CHADEMA.
    Tunafaham fika kuwa katika taasisi yeyote ile, lazima kuna kamati tendaji inayosimamia taasisi hiyo. CHADEMA ni taasisi na ina kamati yake ya Utendaji [ KAMATI KUU] ambayo inakuwa chini ya Mwenyekiti na wajumbe. Bila maamuzi hutolewa na kamati kuu ikijumuisha wajumbe wote. Kwasababu hiyo ili jambo lipite bila shida na ambalo halitaweza kuleta utata kamati kuu inapaswa kuridhika na supporting Reasons ya maamuzi juu ya jambo husika.

Jana Kamati kuu ilimvua Zitto Zuber Kabwa nyadhifa zote za uongozi ndani ya CHADEMA, hakuwa Zitto pekee yake pia wamo Dk. Kitila [ mjumbe kamati kuu ], Shibuda etc kwa madai kuwa wanakisaliti Chama na wanatumika na CCM kuiua Chadema, hoja hii ilipokelewa kwa mbwembwe na shangwe kwa madai kuwa kamati kuu iko sahihi bila kuangalia yatakayokuja mbeleni.

Wakati WANA-CHADEMA wakiwa wanaendelea kuyafurahia maamuzi ya kamati kuu jioni ya saa 11:22 Makamu Mwenyekiti bara Said Arfi aliiandikia CHADEMA barua ya kujiudhuru wadhifa wake, kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kuchoka na unafiki na kuchaguliwa marafiki. Wakati Watu wakianza kutaharuki juu ya barua hiyo. Mjumbe wa tume ya uchaguzi kupitia CHADEMA Pro. Baregu alitoa kauli ya kujiudhuru Kuwa mjumbe wa kamati kuu. Na watu wamebaki midomo wazi juu ya kitu gani kinaendelea ndani ya CHADEMA. Na je maswali ya kujiuliza ni Je wote hao ni wasaliti??? Na kama sio wasaliti ni kwanini viongozi wengine hawahoji yanayotokea?? Wanamwogopa nani, Mbowe, Slaa au Mtei??? Chaajabu maamuzi yote yanayotolewa wanachama wa CHADEMA wanayapokea tu na hamna anayehoji juu ya kwanini yanatokea haya. wao kila kitu ni YES, WELL DONE MBOWE & SLAA, PEOPLESSS,.... POWER

Ndio maana nasema VIONGOZI, WANACHAMA NA WAFUASI WA CHADEMA NI WOGA.

Related

SIASA 292538336983948312

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item