GARY NEVILLE: NATUMAINI SNEIJDER ATATUA OT





Mchezaji wa zamani wa Manchester United Gary Neville anaamini Wesley Sneijder atatua Old Trafford this summer.
United wamekuwa wakihusishwa sana na usajili wa Sneijder ambaye aliisaidia Inter Milan kushinda treble mwaka 2010, pamoja na kuisadia Uholanzi kufika fainali ya WOZA 2010.
Kauli ya Gary Neville inafuatiwa baada ya last week kocha msaidizi no.2 wa United Rene Meulensteen kusema haoni mchezaji mwingine sahihi wa kujiunga na Red Devils kwa wakati huu kama sio Wesley Sneijder.
Alisema: “Sneijder ni mchezaji mzuri ambaye amewahi kucheza katika timu kubwa kama Real Madrid na sasa Inter haitonishangaza akijiunga nasi hapa.
Ana uwezo wa kucheza mahali ambapo ni vigumu kucheza, anaweza kufunga mabao na kutoa assist kwenye mechi muhimu.
Utakuwa ni usajiri muhimu akijiunga na United, lakini na hakika zipo timu nyingine zinamfuatilia.
Natumai Manchester watampata japo sina uhakika na suala hilo.” –alimaliza Gary Neville
Wakati huo huo Wesley Sneijder amezungumzia usajili wake kwenda United huku akisema atahuzunika kama Inter wataamua kumuuza.
“Ningependa kuendelea kubaki hapa, nina team-mates wazuri sana.Mke wangu Yolanthe na mimi tunaipenda Inter, mashabiki na nchi ya Italia.
Ikiwa klabu itaamua kuniuza, nitaenda popote watakaponipeleka lakini itaniuma sana.
Mimi na familia yangu tumekuwa tukijisikia vizuri tukiwa hapa, na nitaumisi sana mji wa Milan pamoja na Inter.Lakini soka ndio lipo hivyo, kipindi ambacho nilipouzwa na Real Madrid kuja Inter, nilitamani kuendelea kubakia nchini Hispania.
Chochote kitakachotokea, kitatokea.” – alimaliza Sneijder

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item