simba wanatisha
https://menacotz.blogspot.com/2011/07/simba-wanatisha.html
VIGOGO wa soka nchini, Simba jana walifanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Kombe la Kagame.
Simba imetinga fainali huku kipa wake, Juma Kaseja akiwa shujaa baada ya kupangua mkwaju wa penalti uliopigwa na Jonas Sakwaha na kuivusha timu yake hadi fainali kwa mikwaju 5-4.
Mshindi katika mechi ya leo kati ya Yanga na St George ndiye atakutaka na Simba katika fainali itakayochezwa keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
“Timu imecheza vizuri, wachezaji wamecheza vizuri kwa kuwa wanabadilika, hilo ni jambo la faraja kwangu, nitaendelea kukiandaa kikosi kwa ajili ya mechi ya fainali kati ya timu yoyote itakayoingia fainali kati ya Yanga au St George,” alisema Kocha Mkuu wa Simba, Moses Basena (pichani), raia wa Uganda.
Akielezea mchezo huo kocha wa El Mereikh, Hossam El Badry kutoka Misri alisema: “Nasikitika kwa wachezaji wangu kukosa nafasi za wazi ambazo tulizipiata kutokana na makosa ya mabeki wa Simba.”
Katika mchezo huo, El Mereikh ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 12 kupitia kwa Adiko Rime ambaye alimalizia krosi iliyopigwa na Sakwaha baada ya kuwatatiza mabeki na kipa wa Simba, Juma Kaseja.
Simba ilisawazisha bao hilo dakika ya 24 kupitia kwa Ulimboka Mwakingwe aliyemalizia kwa kichwa krosi kutoka kwa Shija Mkina.
Matokeo ambayo yalidumu hadi dakika 90 na baadaye 30 za nyongeza, mwisho ikawa ni mikwaju hiyo ya penalti.
Walioifungia Simba mikwaju hiyo ya penalti ni Jerry Santo, Salum Kanoni, Said Nassor ‘Chollo’, Patrick Mafisango, Ulimboka Mwakingwe wakati Salum Machaku, alikosa.
Kikosi cha Mnyama Simba kilikuwa hivi: Kaseja, Chollo, Amir Maftah, Kelvin Yondani, Juma Nyosso, Santo, Mafisango, Shija, Ulimboka, Haruna Mosh ‘Boban’, Mussa Mgosi
Beki wa Simba Amir Maftar(kulia), akiondosha mpira langoni mwake huku akizongwa na beki wa El Mereikh, Badrr Eldin Eldod.
Wachezaji wa El Mereikh wakishangilia goli lao la kwanza sambamba na wapenzi wa Yanga walioko jukwaani.
TIMU ya Simba ya jana iliingia fainali ya Kombe la Kagame kwa kuitoa El Mereikh ya Sudan katika mchezo wa kukata na shoka uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo dakika tisini zilimalizika kwa sare ya bao 1-1. Ziliongezwa dakika 30 lakini hakuweza kupatikana mbabe, ndipo ikabidi yapigwe matuta (penalti) ambapo Simba waliibuka washindi kwa mabao 5-4.
TIMU ya Simba ya jana iliingia fainali ya Kombe la Kagame kwa kuitoa El Mereikh ya Sudan katika mchezo wa kukata na shoka uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo dakika tisini zilimalizika kwa sare ya bao 1-1. Ziliongezwa dakika 30 lakini hakuweza kupatikana mbabe, ndipo ikabidi yapigwe matuta (penalti) ambapo Simba waliibuka washindi kwa mabao 5-4.
Ulimboka Mwakingwe, akiwachambua mabeki wa El Mereikh.
Kipa wa El Mereikh, Isam Elhadary, akibinuka na kuuangalia mpira unavyongia golini ukitoka kichwani mwa Ulimboka Mwakingwe (nyuma yake).
Mashabiki wa Simba wakishangilia baada ya Ulimboka kusawazisha bao
Post a Comment