wema sepetu vs diamond ni nomaaaa
https://menacotz.blogspot.com/2011/07/wema-sepetu-vs-diamond-ni-nomaaaa.html
Na Luquman Maloto
Shugamami, Wema Isaac Sepetu amenaswa live ‘akimbemenda’ serengeti boy, Naseeb Abdul ‘Diamond’, kila kitu kinajieleza kwa picha.
Wema katika mapito yake ya kimapenzi ameweka rekodi ya kuwa na wanaume mbalimbali, hivyo uzoefu wake kwenye ‘yale mambo yetu’ ni mkubwa kwa maana hiyo mbele ya Diamond yeye ni sawa na shugamami ‘anayembemenda’ serengeti boy.
The Udaku Master, Ijumaa linamiliki ‘kabrasha’ la picha za Diamond na Wema ambazo inadaiwa walipiga ‘geto’ kwao wakiwa kimahaba zaidi.
Picha hizo ambazo Ijumaa limezinasa mtandaoni, Wema na Diamond wanaonekana wakiwa kwenye hisia kali za kimapenzi, baadhi zina viashiria vya juu vya ngono, kwa hiyo Ijumaa limezingatia maadili katika ‘kuzipiga chini’ na kutumia zenye afadhali.
Siyo stori kwamba Wema na Diamond ni wapenzi ila kinachotengeneza kichwa cha habari ni picha hizo ambazo nyingine hazina heshima, kwa hiyo zinawaondolea sifa ya kuwa kioo cha jamii.
Kwa mastaa wanaopaswa kuigwa na jamii, picha za viashiria vya ngono ingekuwa mwiko kwao.
DIAMOND NI NANI?
‘Bwa mdogo’ Diamond, alianza kujulikana mwaka 2009 alipotoa kibao chake ‘Kamwambie’ ambacho kilimtambulisha vema kwenye jamii kiasi cha kumuwezesha kunyakua tuzo tatu za Kilimanjaro Tanzania Music Awards mwaka jana kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Dogo huyo ambaye siyo uongo kwamba anajua kuimba, ghafla alidondokea kwenye penzi la Staa wa Filamu Bongo, Jacqueline Wolper ambaye hata hivyo alikanusha na kila akikumbushiwa stori za Diamond huwa anakuwa mkali.
Warembo Upendo Moshi aliyeshiriki Shindano la Maisha Plus Season II na mshiriki wa Miss Kiswahili 2009, Rehema Fabian wote wamewahi kujitangaza kutoka kimapenzi na Diamond.
VIPI WEMA?
Kwa ‘mdada huyo’ ambaye alinyakua Taji la Miss Tanzania mwaka 2006, amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na wanaume kadhaa ambao wengine wana umri mkubwa.
Wema ‘ameshashea’ uzoefu wa kimapenzi na Mkurugenzi wa Hartmann Production, Hartmann Mbilinyi ambaye ni mtu mzima na kwa umri anaweza kumzaa Diamond.
Kipimo kimoja tu cha Wema kupata uzoefu wa penzi la Hartmann kinatosha kutoa tafsiri kuwa Miss Tanzania huyo mwenye skandali nyingi, anapoangukia kwa Diamond leo ni sawa na ‘kumbemenda’.
CHEKI WANAUME HAWA
Wakati kabla ya Wema Diamond anahusishwa na wanawake watatu, kwa mrembo huyo kuna mlolongo wa tuhuma.
Wema amewahi kudaiwa kutoka kimapenzi na wakali wa Bongo Fleva, Khaleed Mohamed ‘TID’ na Heri Samir ‘Blu’ ambao ni makaka wakubwa wa Diamond kuanzia umri mpaka ustaa.
Wakati Diamond anaitafuta miaka miwili tangu aanze kupata jina mjini, TID ‘Mjelajela’ ana zaidi ya miaka 10 hewani, wakati Blu yeye anatusua kwa mwaka wa nane sasa.
Miss Tanzania huyo anadaiwa pia kutoka kimapenzi na mastaa wakubwa Bongo, Steven Kanumba, Charles Gabriel Mbwana ‘Charlz Baba’ na Jack Pemba ambao nao wapo hewani kwa miaka mingi na kwa umri ni makaka wa Diamond huku Jack kwake inawezekana hata kumzaa.
Wema pia anadaiwa kuwahi kutoka kimapenzi na wanaume wenye umri mkubwa mbele ya Diamond, Jumbe Yusuf na Paul Masoud ambaye ni Mtanzania anayeishi Marekani.
Katika mwendelezo wa matukio ya kimapenzi ya Wema, ‘mdada’ huyo anadaiwa kuwahi kutoka kimapenzi na mbunge mmoja wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (jina tunalo) ambaye siku akikutana na Diamond ni lazima amtangulizie shikamoo.
UMBO
Pointi nyingine ambayo inamfanya Wema aonekane ‘anambemenda’ Diamond ni umbo lake ambalo ni kubwa.
Wema ni mrefu, mnene tofauti na Diamond ambaye hana ‘supu’, kwa hiyo ni mwembamba na kuhusu kimo, inabidi asimamie vidole ili alingane na mlimbwende huyo.
Tofauti hiyo ya maumbo inafanya Wema aonekane anambemenda Diamond kila wanapokuwa pamoja.
KUTOKA IJUMAA
Ni vema Diamond akatambua kuwa huyo ndiye Wema a.k.a mfupa uliomshinda Kanumba, Jumbe, Charlz Baba na wengine ambao waliamini wangefunga ndoa, kwa hiyo pamoja na kumpenda anapaswa kulinda heshima yake na ya familia yake.
Hulka ya kupiga picha za chumbani na kuziweka hadharani siyo sawa. Haivutii mbele ya jamii na zaidi inawachafua na kuwaondolea sifa ya kuwa kioo cha jamii.
kwa hisani ya globalpublishersI

Post a Comment