HICHI NDICHO WALICHOSEMA MASHABIKI WA RAY KWENYE BLOG YAKE BAADA YA KIFO CHA KANUMBA


25 comments:

Anonymous said...
RAY POLE DUUU UMEJIKAZA SANA UTAKUWA UNAMLIZA HUYO MAMA KILA SIKU TUOMBA UJITAHIDI KUWEKA PENGO KWA MAMA KIDOGO ITASAIDIA POLE NDUGU YANGU.
Anonymous said...
POLE SANA RAY
Anonymous said...
Ray nimekutumia msg facebook usipublish kwasababu ni personal msg yako na johari plssssss just for the seek of me marry her,nampenda johari ni mke siunaona hawawanawake wengine ni wasumbufu tu plsssss do it fo me as ur big fan u have my facebook name siku ikiwa hivyo pls invite me and i will contribute the little i will manage.nataka ubadilishe maisha kwa mtazamo tofauti ukiwa mume heshima inabadilika na sasa hivi taifa limetambua umuhimu wa wasaniii kwa ndio nchi wanaweza kugeuza nchi kabisa.kanumba wil be so proud of u bro
Anonymous said...
POLE SANA KAKA RAY MUNGU AKUZIDISHIE KWA YOTE ULIO MTENDEA NDUNGU YAKO KANUNUMBA LAKINI NDUNGU YANGU BADILIKA WEWE SIO KAMA MAREHEMU UNAMAJIDAI SANA JAPO TUNAPENDA KAZI ZAKO LAKINI HUNA MAPENZI NA SIE KAMA ALIVYO KANUMBA SIUMEONA JINSI KANUMBA ALIVYO ZIKWA NA WATU NI KWA AJILI YA ROHOYAKE YA KUSAIDIA WATU NA UPENDO ALIOKUWA NAOKWA WATU
Anonymous said...
Pole saana tena saana kaka Ray. Mwenyezi mungu atujalie subira na nguvu ktk kipindi hiki kigumu. Mipangi ya mungu haina makosa muhimu ni kuwa waja wema na tuombeane kwa mungu na kupendana kwa dhati. R.I.P Kanumba.


Anonymous said...
pole sana ray ni hakika hatujui unajisikiaje sasa hivi kwa kanumba kuondoka Mungu yeye anayajua yaliyoko mioyoni mwetu,pole kaka.
Anonymous said...
POLE BRO those are challenges that human beings faces bt b storng iknw people will talk more kama u were are a good friend ull alwayas b my brother
Anonymous said...
pole sana Ray, mimi nikiangalia tu hizi picha nalia tu lakini wala simjui kanumba wala sijawahi kuona movie zake ila, ameondoka bado kijana sana na taifa linamwitaji, kama marafiki zake pia msimwache LULU kwa sasa hamjui kilichotokea RIP KANUMBA
Anonymous said...
RAY MBONA SIJAONA NI JINSI GANI UMEUMIA KUHUSU KIFO CHA KANUMBA?KWANZA MUDA WOTE UMEVAA TU MIWANI HATA SIJAKUELEWA, NA JE NI KWELI WE NA KANUMBA MLIKUWA NA UGOMVI?ANYWAY POLE SANA RAFIKI YANGU MIMI BINAFSI NIMEUMIA SANA SANA TULIMPENDA SANA KANUMBA ILA MUNGU KAMPENDA ZAIDI, REST IN PEACE KANUMBA
Anonymous said...
SASA UNA MAMA WAWILI... HAKIKISHA UNAFANYA HIVYO MPAKA MWISHO WA UHAI WAKO NA KAMA AKIRUDI BUKOBA UWE UNAENADA KUMSALIMIA.
nacho kusifu HUJIBISHANI NA MTU KWENYE BLOG WW UNASOMA COMMENT NA KUFANYA KILE UNACHOKIONA NI SAHIHI
huwezi kuridhisha kila mtu..
watu wanaweza kuponda kuwa urifurahi kwenda kununua jeneza ili umtoe haraka dunia.... watu jamani.
ALAFU SAMAHANI RAY,, nimeona picha za mama kanumba alizoenda makaburi leo(millard ayo),, sijamuona mama yako kwani mama yako kaisha ondoka msibani inabidi awem naye karibu maaana inawapasa waitane mtu na dada. ampe kampani yakutosha. wakibaki na wanae du HATARI
emmer matutu
Anonymous said...
Endeleo kuonyesha upendo kwa mama kanumba.na endelea kumuenzi swahiba wako kwa kuhakikisha kazi zake zinatoka alizoanza.na kampuni yake.pia uwe unamtembelea pale makaburin kndoni.
Anonymous said...
kweli msiba huu umetuumiza wote.... sijui sinema zake alizoacha kama watu watamfanyia unyama au watakuwa waukweli....

Pumziko la milele umpe eeeh bwana...

Kanumba the great
Anonymous said...
wewe Ray ni mnafiki,kilichokufanya uwe kimbelembele hivyo ni nini?inajulikana kabisa haukuwa vizuri na marehemu,sasa kilichokuwa kinakushughulisha hivyo ni nini jamani?naomba kama hujausikiliza mwimbo wa marehemu basi nenda kausikilize,ile msg ilikuwa yako na hao wajinga wenzio hukutakiwa hata kusogelea jeneza la marehemu,hivi ingetokea pale aamke na kukuambia usibebe jeneza lake ungesemaje?shame on u you are time is running out so watch out.
Anonymous said...
hata usipoiweka utakuwa umeisoma kimya kimya kauzu wewe.
Anonymous said...
Mungu ndie anajua unachomuwazia swahiba wako ni vema kama mlkuwa mmemalza tofauti zenu!Au lah!!!!!Ila maisha n kama gwaride kaka yangu pambana ila jua kuna leo na kesho ametangulia Kanumba sote tu nyuma ake its better ukajipanga ili kuswe na utata kama uliopo now!!!!!!!!!!!!!!
Anonymous said...
Laiti 2ngekuwa 2meumbwa kwa vioo au sightmirror 2ngeona yale wenzetu wanatuwazia dah niliipenda hii ila ndo hivyo man unajua unachomuwazia Marehemu swahiba wako cha kufanya mkumbuke ktk sala zako uombe msamaha pale mliposhndwana I believe Mungu atakuskia!!!!!!!!!keep it up Ray
Anonymous said...
wanaadamu tuache kuhukumu,pole sana ray
Anonymous said...
RIP Kanumba wl olways remember you!!!!!!Ray please jitahidi katika kazi kazo na umwombe na kumwamini Mungu aliye hai ndo kimbilio letu wanadamu,wengine hao sio kabiiiiiiiisa!!!!!!!
Anonymous said...
Sasa jamani Ray anatukanwa kwanini? Kanumba alisisitiza upendo hivyo basi ingekuwa vyema kama tungemuenzi kwa kuonyesha upendo kati yetu. Just leave Ray alone people, if u dnt have anything nice to say then just dont.
Anonymous said...
Kwa nini ulijiita THE GREATEST baada ya kuona kanumba anajiita THE GREAT.....?
Hilda canada. said...
Nimefurahi kumwona mama yako akimfariji mama wa kanumba huo ni upendo wa dhati.Mi bado sijaelewa kuna watu wanasema huna majonzi eti umevaa vizuri na miwani jamani tuache kumnyima amani huyu kijana ina maana alitakiwa abebwe ndo uchungu uonekane?Kuwa smart siyo dhambi jamani ila uchafu ni dhambi.Wote mlioko huko na sisi tulio mbali wote tulipata huzuni kwa kuondokewa na kijana mwenzetu akiwa bado na ndoto zake nyingi. bado mdogo. Ni vizuri tutiane moyo kwani nani anajua saa yake ya kuondoka?
judy canada said...
Nikupe pole na nikusifu kwa kujikaza na kujishughulisha kwa ajili ya mpendwa wetu Kanumba. Kujitoa kwenye msiba sio ili watu wakuone ila unajikuta unajishughulisha kwa ajili ya mapenzi na upendo kwa aliyeondoka.Siyo kwamba ukishughulika sana huna majonzi la ila kama una nguvu ni vizuri kujitahidi na ndivyo ulivyofanya. Huo ni upendo pia kwa wafiwa najua ukifiwa unakosa nguvu so isingekuwa vizuri wadoge zake wakatafute jeneza na nyie marafiki mpo.Tusiwe wahukumu tukumbuke pamoja na mapenzi makubwa tuliyokuwa nayo kwa kanumba hakuna mtu angekubali azikwe kaburi moja na yeye. Wote tungekimbia kama tulitakiwa kuonyesha huzuni kwa kuzikwa pamoja.Tufarijiane. upendano husitiri wingi wa dhambi.
canada said...
Hili ombi ni kuhusu hao dada zenu wa bongo movie.Wekeni wazi mambo yenu aliye na mchumba amweke wazi kabla haujaja mda yatajianika wazi kwa njia isiyo nzuri. Nyinyi wote ni watu wazima kwa nini mnafichaficha mahusiano yenu kama watoto wa shule ambao wanaogopa baba asijue? Jengeni heshima kwa jamii kwani kuna watu wanawapenda na kufurahia mafanikio yenu. Baadhi ya dada huko bongo movie hata ukiwapa Hi anakausha kisa s tar hao mnaowakaushia mtaani mkipata matatizo makubwa si ndiyo hiyo hiyo jamii mnaiomba msaada??Msichague uso wa kupokea salam Mtu anapokupa salamu hakuombi hela wala hupungukiwi na kitu, heshima haiuzwi.Hujui ni tatizo gani litalokufanya uombe msaada kwa hao hao ambao si star inaweza kuwa ugonjwa au case mbaya unajikuta kuna watu wangeweza kukusaidia ila kwa sababu ulionyesha dharau na kiburi wanauchuna tu.
Anonymous said...
watanzania mna maneno, eti ule wimbo wa KANUMBA ALIMTUNGIA RAY je wasingetofautiana na RAY HUO WIMBO MNGESEMA WA NAN? ME NADHANI HAWAKUWA NA BIFU LA KIHIVYO KM MAELEWANO HAYAKUWEPO BAS N YA KIBINADAMU TU KM MNAKUMBUKA KUNA GAZETI LILITOKA RAY AKIMSHAUR KANUMBA AMALIZE TOFAUT NA BABA YAKE, LIKATOKA TENA GAZETI LIKASEMA KANUMBA AMESEMA "RAY UNANITAFUTA UTANIPATA" LKN BAADA YA HAPO KANUMBA ALICHUKUA LILE GAZETI AKAWEKA KWNYE BLOG YAKE AKASEMA YY KANUMBA HAJASEMA HAYO MANENO SS HAMUON KM HAKUKUWA NA UGOMVI MKUBWA KIIVYO NA NDO MANA KANUMBA ALIKANUSHA YALE MANENOO EM KUWENI NA AKILI BWANA INGIENI KWNY BLOG YA KANUMBA MKAANGALIE KWNY OLDER POST MTAELEWA NNACHOMANISHA, muacheni RAY WA WATU HATA KM HAMUMPEND TUPO TUNAOMPENDA NA BNADAM ALOKAMILIKA HAWEZI KUPENDWA NA WATU WOTE AU KUCHUKIWA NA WATU WOTE.
Anonymous said...
Nimekupenda sana Ray, wewe ni msanii, kwa jinsi ulivyopangilia story ya Kanumba kwenye blog yako inaonyesha ni jinsi gani ulivyo msanii, umeanzia mwisho kuja mwanzo. Waandishi wengi wa vitabu kutoka Nigeria wanapenda kuandika kwa mtindo huo. Nimegundua kitu, kuwa wewe na Kanumba hamkuwa marafiki tu bali ni NDUGU kabisa, kama urafiki wenu ulifikia hata mpaka wazazi nao ni marafiki jamani. Big up sana Ray.Hivi Watanzania mnataka Ray afanye nini ili mjue kuwa aliumia sana na msiba huu?? Vumilia tu kwa sasa kwa kuwa binadamu ndivyo tulivyo, ni wanafki kuliko unavyofikiria, hata kwenye msiba wa Kanumba, najua ni wengi wangeumbuka kama Kanumba angeamka japo kwa dakika 5 tu. Unakumbuka ile redio iliyomtengenezea matangazo ya kumuaibisha kuwa aliongea kingereza kibovu alivyoenda Big Brother? uliona jinsi walivyokuja kuwa wanafki eti siku nzima ya mazishi yake hawakuwa na vipindi vyovyote zaidi ya kutangaza kuhusu Marehemu Kanumba. Kuwa na bidii siku zote na usiwasikilize watu, sisi binadamu ni wanafki sana. Mi napenda kukutia moyo usiangalie nyuma tenda wema uende zako, endeleza tasnia, utafika mbali.
RIP Kanumba.

Ni mimi mpenda maendeleo yako
Mzalendo halisi.

Related

Celebrities 245441399717921472

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item