OKWI KUTUA DAR NA KIUNGO MPYA WA SIMBA



Emmanuel Okwi.
Na Khatimu Naheka
MSHAMBULIAJI tishio wa Simba, Emmanuel Okwi, anatua nchini leo sambamba na kiungo mpya wa timu hiyo, Mussa Mudde. Mudde, raia wa Uganda, ni moja ya sura mpya zitakazoonekana katika msimu ujao zikiwa na uzi mwekundu, akitokea Sofapaka ya Kenya. Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, amesema Okwi anatarajiwa kutua nchini leo akitokea kwao Uganda akiwa na Mudde. “Okwi anakuja na Mudde, baada ya kutua wataungana na wenzao moja kwa moja katika maandalizi ya msimu mpya wa ligi ambao utatanguliwa na michuano ya Kagame itakayofanyika hapa nchini,” alisema Kamwaga. Mudde ambaye alikuwa tegemeo la Sofapaka ya Kenya na timu ya taifa ya Uganda, The Cranes, ameshamalizana na Simba na Championi ndiyo lilikuwa la kwanza kuandika kuhusiana na kujiunga Msimbazi. Okwi anatua kwa ajili ya kukamilisha taratibu kabla ya kwenda kwenye majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Italia au Afrika Kusini kwenye Klabu ya Orlando Pirates.

CHANZO NI: CHAMPIONI JUMATANO

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item