HATIA--07
https://menacotz.blogspot.com/2012/10/hatia-07.html
Na George Iron
Moshi wa bangi na sigara vilianza kuizoea
damu yake, sumu ya maneno aliyokuwa akilishwa na John Mapulu sasa ilikuwa
imesambaa ndani ya damu yake, aliwaona watu wote wanaomzunguka kuwa ni maadui
hasa hasa askari.
John alimwelezea Michael jinsi polisi
wanavyoua raia wema hovyohovyo, alimpa mikasa mbalimbali ya kutisha hivyo
kuikoleza hoja yake kuelekea kwenye ukweli. Taratibu Michael akaanza na sigara
hatimaye akajiunga katika mkumbo wa wavuta bangi, kwa jitihada zote aliyapinga
matumizi ya unga hilo pekee ndilo alilipigania hadi mwisho.
Mwanzoni alikuwa msindikizaji katika
shughuli walizokuwa wakienda kufanya akina John sehemu mbalimbali katika jiji
la Mwanza kila baada ya shughuli alipewa nafasi ya kuuliza maswali mawili
matatu. Kwa kuwa Michael alikuwa mwingi wa maswali hii ilimuwezesha kuelewa
mambo mengi sana katika kipindi kifupi mno.
Tayari alijua mbinu za kuvunja maduka,
kuiba magari, na mbaya na kubwa somo la matumizi ya silaha lilikuwa limemkolea.
John Mapulu hakuwa mtu wa masihala
linapokuja suala linalomuhusu moja kwa moja, jambo hili hata Michael alilitambua
upesi sana kadri alivyokuwa akiishi naye karibu. Mahusiano yaliyokuwepo kati
yake na Matha (mpenzi wa John) katika kufundishwa jinsi ya kutumia bunduki
yalikuwa yameanza kuvuka kiwango, nafsi ya Michael baada ya kumtamani Joyce
Keto bila mafanikio ya kumpata, Joyce mwingine aliyefariki bila kuwa ameelewa
azma ya Michael, sasa Michael alikuwa anamtamani Matha japo pia alikuwa
hajamwambia, kila siku alikuwa akijizuia na kuuonya mdomo wake usije ukamponza.
Aliamini kwa kumtamkia Matha kuwa anampenda
ni sawa na kuanzisha vita na John Mapulu, vita kubwa ambayo wala hakuwa na
ubavu wa kuicheza. Wakati fulani Michael aliamini Matha amewekwa karibu yake
ili kumchunguza tabia zake hivyo alikuwa makini sana asiweze kuzionyesha hisia
zake kwa mrembo huyu.
Matha hakuisha kumvalia nguo za mitego
Michael kila wanapokuwa wawili katika chumba maalumu cha mafundisho hayo.
Siku hii jioni tulivu kabisa John na
wenzake wakiwa wameingia katika tukio la kuiba pesa benki ambapo hawakutaka
kuandamana na Michael kwa sababu ya uchanga wake katika masuala ya uharifu pia
hawakuwa na mtaalamu wao wa kike Matha Mwakipesile aliyedai kwamba akili yake
haikuwa barabara siku hiyo. Michael kama kawaida akiwa katika burudani yake ya
kuangalia filamu, mwilini akiwa na pensi fupi na fulana iliyokatwa mikono
alishtuliwa ghafla na ujio wa Matha pale ndani.
“He!! Mwalimu vipi….pole aisee nasikia
unaumwa??.” Michael alimuanza Matha ambaye kwa sasa walikuwa wamezoeana sana.
“Mh!! Kakwambia nani??”
“Ah!! Nimesikia tu!!!” alijibu huku
akisimamisha hiyo filamu kupisha maongezi yake na Matha.
SOMA HADITHI KAMILI HAPA >>>>>>>
Post a Comment