SITAISAHAU facebook!

SEHEMU YA KWANZA               1

MTUNZI: Emmy John P.

MAWASILIANO: 0654 960040

“Isabela….Isabela…” nilisikia sauti ya mwanamke ikiniita, niligeuka mara moja maana sauti ile ni kama niliwahi kuisikia mahali. Lakini sikukumbuka ni wapi. Giza totoro lilinizuia kuweza kumtambua mtu yule aliyeniita kwa ufasaha kiasi kile tena gizani. Nilianza kujiuliza iwapo nirejee nyuma kurudi kumtafuta ama niendelee mbele ambako pia sikuwa na uhakika ni wapi. Manyunyu ya mvua yalikuwa yamenilowanisha hasa na nguo yangu ilikuwa imeshikana na mwili. Nilikuwa natetemeka huku michubuko kadhaa katika mwili wangu ikiniwashawasha. Kilikuwa kitendawili aidha niende mbele ama nirudi nyuma kuifatiliza hiyo sauti. Ile hali ya kujiuliza niende mbele ama nirudi nyuma ikanifanya niwe kama naigiza igizo lisilokuwa rasmi. “Isabelaaaa!!!.” Iliita tena sauti hii. Sasa ilisikika dhahiri kuwa sauti ile ilikuwa katika kulia, mwenye sauti ile alikuwa katika uchungu mkubwa na bila shaka aliuhitaji sana msaada wangu. Nilitamani kuitika lakini midomo ikawa mizito. Nilipolazimisha kuitika nikawa kama nanong’oneza, sauti haikutoka. Koo lilikuwa limekauka sana. Hapo ndipo nikagundua kuwa nilikuwa na kiu sanaSOMA HADITHI KAMILI HAPA >>>>>>>>>>>

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item