ASKARI ALIYEPIGA PICHA NA LEMA AHUKUMIWA MIAKA 4 JELA
https://menacotz.blogspot.com/2013/01/askari-aliyepiga-picha-na-lema.html
Mbali na kupiga picha hiyo na Lema
pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari, kijana huyo
alionekana katika picha hiyo akionyesha vidole viwili, ambayo ni alama
ya Chadema.
Hata hivyo, baada ya picha hiyo, JWTZ
lilimtilia shaka kijana huyo na kutangaza rasmi kumsaka, ili
lijiridhishe kama ni mmoja wa wanajeshi wake.
Jana, Kikulu alifikishwa mahakamani
mjini Moshi, akiwa chini ya ulinzi wa polisi na kusomewa mashtaka
mawili, ambayo yote alikiri kuyafanya kama ilivyodaiwa mahakamani.
Katika shtaka la pili,
wakili huyo alidai siku hiyo hiyo katika Mtaa wa Msikitini, eneo hilo
la Bomang’ombe, mtuhumiwa alipatikana na sare za JWTZ kinyume cha
sheria.
Sare hizo ni pamoja na suruali moja,
mashati mawili na kofia mbili, vyote vikiwa na alama za Jeshi la
Wananchi wa Tanzania la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kutokana na kukiri kwake makosa hayo,
Hakimu Kobelo alimhukumu kifungo cha miaka miwili kwa kosa la kwanza la
kujifanya Ofisa wa JWTZ na miaka mingine miwili kwa kosa la pili.
Kwa mujibu wa hakimu huyo, kosa
alilolifanya mtuhumiwa huyo ni baya na linastahili adhabu kali, ili iwe
fundisho kwa watu wengine wanaotumia vibaya sare za majeshi nchini.
Baada ya kumsaka kwa takriban siku 12,
kijana huyo alikamatwa Januari 3, katika Mji wa Bomang’ombe wilayani
Hai na baada ya kupekuliwa alikutwa na sare hizo.
Baada ya kukiri kosa hilo Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Kilimanjaro, alimhukumu kifungo cha
miaka minne jela, ili iwe fundisho wa wakosaji wengine wa aina hiyo.
Kabla ya hukumu hiyo, Wakili wa
Serikali, Ignas Mwinuka alimsomea mshtakiwa huyo mashitaka yake mawili,
likiwamo la kujifanya Ofisa wa Jeshi, wakati akijua ni uongo.
Wakili huyo alidai mahakamani kuwa
Januari 3, mwaka huu katika eneo la Bomang’ombe wilayani Hai, mtuhumiwa
huyo alijitambulisha kama mtumishi wa umma.
Baada ya Hakimu Kobelo kumuuliza
mshtakiwa kama ni kweli alitenda makosa anayoshitakiwa, mshtakiwa huyo
alikiri makosa yake katika hali ambayo haikutarajiwa.
Hata hivyo, Hakimu Kobelo alisema kuwa
kwa kuwa adhabu hizo zinakwenda kwa pamoja (concurrent), mshtakiwa
huyo atatumikia kifungo cha miaka miwili jela.
Post a Comment