BBC:Wafaransa wapinga ndoa ya jinsia moja
https://menacotz.blogspot.com/2013/01/bbcwafaransa-wapinga-ndoa-ya-jinsia-moja.html
Maelfu ya Wafaransa wameandamana katika barabara za mjini Paris kupinga mpango wa serikali kuhalalisha ndoa kati ya jinsia moja.
Watu kama laki moja wameandamana katika mihadhara mitatu tofauti na kukusanyika karibu na Eiffel Tower.
Waliotayarisha maandamano hayo wanasema waliohudhuria ni nusu milioni.
Watu walitoka sehemu mbali-mbali za nchi kwa mabasi maalumu yaliyokodiwa pamoja na treni kwa sababu wanaona mpango wa serikali kuhalalisha ndoa kati ya watu wa jinsia moja na kulea watoto, utaharibu msingi muhimu wa jamii.
Bunge linatarajiwa kujadili mswada huo baadae mwezi huu.
Maandamano yanaungwa mkono na kanisa la Katoliki na upande wa upinzani wa mrengo wa kulia.
Lakini wasemaji wanashikilia kuwa maandamano hayo siyo ya kisiasa wala ya kidini na wala hayawalengi wapenzi ya jinsia moja.
Maandamano hayo ni upinzani mkubwa kabisa dhidi ya Rais Hollande tangu kuingia madarakani mwezi wa May.
Post a Comment