MANCHESTER UNITED YAINYUKA TENA LIVERPOOL 2-1 OLD TRAFORD

>> KWENYE MECHI YA SUPER SUNDAY

>> KUWA MBELE POINT 10 (KABLA YA MECHI YA ARSENAL v MANCHESTER CITY)


        katika mechi ambayo ilikuwa ngumu na ya kusisimua , timu ya Manchester United imeiibuka kidedea mbele ya vijogoo vya Anfield baada ya kuwachapa Magoli 2-1. Man U ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Liverpool kupitia kwa muuaji wao hatari Robin Van Persie mnamo dakika ya 16', goli ambalo lilidumu hadi mapumziko ambapo walikuwa Man U tena ambao walijipatia goli kupitia kwa Evra ambaye alifunga kwa kichwa baada ya faulo ambayo ilipigwa na RVP. hata hivyo Liverpool walijipatia goli lao la kufutia machozi kupitia kwa Sturridge ambaye alitokea Bench baada ya piga nikupige langoni mwa Man United. hadi dakika 90 zinaiisha Man U 2-1 Liverpool

       Pamoja na mechi kwisha hivyo,ila mechi ilikuwa imebalance maana Man United walicheza vizuri kipindi cha kwanza na pia Liverpool walicheza vizuri kipindi cha pili.


    Moja ya matukio makubwa ambayo yalijitokeza kwenye mechi hii ni pamoja na uwepo wa Jose Mourinho pale Old Traford. Kila mmoja alikuwa na lake kichwani kutokana na uwepo wa Kocha huyo wa Real Madrid ya hispania. Real Madrid jana walitoka suluhu na Osasuna kwenye Laliga.

hapa chini ni baadhi ya picha za mechi hiyo
 
RVP NA EVRA
Evra na Suarez wapeana mikono

EVRA NA RVP wakishangailia goli la Pili


goli la pili la Man United

 
Suarez akijaribu kumtoka Vidic
 
JOSE MOURINHO akiingia Old Trafford

Related

Sports 4688852962414142713

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item