CHADEMA WAMESEMA KAULI ILIYOTOLEWA NA NAPE NNAUYE HAINA UKWELI WOWOTE

https://menacotz.blogspot.com/2013/01/chadema-wamesema-kauli-iliyotolewa-na.html
Akizungumzia kauli hiyo Mkurugenzi wa Sera na Mafunzo wa CHADEMA, BENSON KIGAILA, amesema CHADEMA hakiwezi kufa kwa dhana iliyozungumzwa na NAPE, na badala yake Chama hicho Tawala ndicho kinachoweza kufa kutokana na kukabiliwa, na changamoto nyingi ikiwemo ufisadi.
Katika Hatua nyingine CHADEMA kimemtaka Naibu Katibu wa CCM, MWIGULU NCHEMBA, kutoa ushahidi wa kauli aliyoitoa hivi karibuni, kuwa Chama hicho kimekuwa kikipanga mipango ya mauaji na kubanisha kuwa kauli hiyo, imelenga kulidhalilisha jeshi la Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa.
CHANZO: CLOUDS FM
Post a Comment