BREAKING NEWZ: AJALI MBAYA YA PIKIPIKI YATOKEA ISEVYA MAKABURINI -TABORA
https://menacotz.blogspot.com/2013/02/breaking-newz-ajali-mbaya-ya-pikipiki.html
katika hali ambayo iliwashangaza wengi, ni ajali mbaya ya pikipiki ambayo imetokea leo majira ya mchana pale Isevya sokoni, ambapo dereva pikipiki ambaye jina lake halikupatikana haraka alimgonga mtoto mwenye Umri wa Miaka inayokadiria kati ya kumi ama kumi na moja, ajali hiyo ambayo ilivuta hisia za wengi ilisababisha dereva huyo kuumia vibaya na ikabidi akimbizwe hospitalini haraka kwa matibabu,
CHANZO CHA AJALI HIYO.
kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva aliyeshindwa kukontrol pikipiki yake wakati mtoto huyu anakatiza barabara; "Unajua huyu dereva pikipiki alikuwa anaendesha kwa kasi sana, na wakati huo huyu mtoto alikuwa anakatiza barabara, alipoona pikipiki inakuja kasi akaamua kurudi nyuma, kumbe wakati huo na dereva pikpiki aliamua kupitia pembeni na kumgonga mtoto." alisema moja wa mashuhuda aliyeshuhudia tukio hilo.
MAJERUHI
Dereva pikpiki ndio aliyejeruhiwa zaidi na ajali hiyo na hadi MeNaco.com inafika eneo la tukio tayari dereva pikipiki alishakimbizwa hospitalini kutokana na majeraha aliyoyapata ila ilimkuta mtoto aliyegonwa na pikpiki hiyo akiwa ndio ayupo anapakiwa kwenye pikpiki nyingine ili apelekwe hospitali, mtoto yeye hakuumia sana ila alipata majeraha kwenye bega.
MAMA MZAZI WA MTOTO
aliyesadikiwa kuwa mama mzazi wa huyo mtoto alishindwa kusema chochote juu ya tukio hilo zaidi ya kupanda kwenye defenda ya polisi na kuelekea kituoni kuchukua PF3 tayari kwa matibabu ya mtoto.
POLISI WAWASILI ENEO LA TUKIO.
Haikuchukua muda mrefu sana defenda ya Polisi ilifika eneo la tukio na kuipakia pikpiki ambayo iliachwa chini baada ya tukio, na pia ilimpakia mama mzazi wa mtoto huyo na ndugu mmoja wa mama huyo.
WITO WA MeNaco.com KWA MADEREVA PIKIPIKI
tunawaomba madereva pikpiki muwe mnatumia mwendo wa kawaida tu kwani BORA KUCHELEWA UKAFIKA KULIKO KUWAHI USIFIKE.
TUNAWATAKIA AFYA NJEMA MAJERUHI
2 comments
good work kwa habari na nawapa pole wahanga wa ajali hiyo
Good Job Buddy... Keep it up...
Also visit this webpage : The Power Sports
Post a Comment