KLABU BINGWA AFRIKA: AZAM YASHINDA, JAMHURI YACHAPWA NYUMBANI GOMBANI 3-0!

>JUMAPILI: SIMBA KUIKWAA LIBOLO!!

AZAM_FC_PLAYERSKLABU za Tanzania, Azam FC na Jamhuri, zimecheza Mechi zao za kwanza za Mashindano ya Klabu Barani Afrika kwa Mechi za kwanza za Nyumbani na Azam kuiwasha Al Nasir Juba ya South Sudan Bao 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam  na huko Gombani, Chake Chake, Kisiwani Pemba, Jamhuri kutandikwa Bao 3-0 na St George ya Ethiopia.
Huko Pemba, katika Mechi ya Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI ambayo Jamhuri walitandikwa 3-0, Bao za St George zilipachikwa na Omande Ukure, Dakika ya 5, Gabremariam, Dakika ya 54 na Joseph Oguena Dakika ya 79.
Nako Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwenye Mechi ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho, Azam FC walitangulia kupata Bao kupitia Abdi Kassim, Dakika ya 14, na Al Nasir kusawazisha kwa la Fabian Elias katika Dakika ya 38.
Lakini, Bao mbili za Kipre Tchetche, katika Dakika za mwishoni, ziliwapa Azam FC ushindi wa Bao 3-1.
Mechi za Marudiano zitachezwa baada ya Wiki mbili.
Kesho, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mabingwa wa Tanzania Bara, Simba, watacheza na Clube Rec. Libolo ya Angola katika CAF CHAMPIONZ LIGI.

Related

SIMBA SC 8569845779963017220

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item