GAZETI LA MWANANCHI LAPATA MWONEKANO MPYA NA WA KUVUTIA


 Jana usiku, kampuni ya Magazeti ya Mwananchi Communications ilizindua muonekano mpya wa gazeti lake la Mwananchi ambapo ilifanya halfa fupi katika ukumbi wa Mlimani City, hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kiserikali, vyama vya siasa, wafanyabiashara, wadau wa habari  na watu mbali mbali maarufu jijini Dar es salaam. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya marekebisho ya Katiba, Balozi Joseph Sinde Warioba. Pichani juu anaonekana Mheshimiwa Warioba(Wa pili kutoka kushoto, akishiriki katika zoezi la uzinduzi wa gazeti hilo lenye muonekano mpya, pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya kampuni hiyo, Bi Zuhura Muro, huku Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw Tido Mhando(kushoto), na Meneja Biashara na maendeleo, Bw Theophil Makunga(kulia) wakishuhudia
Mhariri Mtendaji wa kwanza wa gazeti la Mwananchi, ambaye kwa sasa ni MenejaMaendeleo ya Biashara akieleza kwa kina kuhusiana na miaka 13 ya Gazeti la Mwananchi na mafanikio yake kwa waalikwa
 Nasaha kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Bw Tido Mhando
 MEZA KUU: Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari, Dk Reginald Mengi, Mgeni Rasmi Mh Warioba, na Mwenyekiti wa Bodi wa MCL Bi Zuhura Muro wakiteta jambo
 Mwenyekiti wa Bodi naye alisema machache
 Mhariri Mtendaji wa Gazeti la mwananchi, Bw Dennis Msacky(kulia), akiwa na Kaimu Mhariri Mtendaji wa kampuni ya MCL,  Bakari Machumu na mtaalam wa ubunifu wa kurasa Bi Kelly Frankeny
 Uzinduzi rasmi...
 ..na huu ndio muonekano mpya!
 Linapendeza kwa kweli
 Umeona mwenyewe, hapa ni kila sehemu ya ndani imefanyiwa marekebisho
 Picha na watu mashuhuri
 Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma kaskazini pamoja na katibu mwenezi wa Chama Cha mapinduzi, Nape Nnauye wakiteta jambo
 
 MCL Team
Meza kuu ilipata nafasi ya kuperuzi, ...na kudadisi...
 Baadae kila mtu alipata nakala yake
 Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari, Dk Reginald Mengi akitoa nasaha zake
kelly Frankey, mtaalamu wa miundo mbali mbali ya gazeti la mwananchi naye alipata wasaa wa kujieleza mbele ya wageni waalikwa
 Kila mtu alifurahi
Mshereheshaji alikuwa Taji Liundi, moja kati ta wakongwe katika tasnia ya utangazaji
Baada ya yote, Skylight Band ikamaliza mambo kwa burudani ya Nguvu!Picha Zote Kwa Hisani ya Mdimu Blog

Related

MWANANCHI 1811000288886731994

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item