NATIONAL HOUSING YAJILIPUA KUHUSU JENGO LILILOANGUKA JUZI BONGO!!
https://menacotz.blogspot.com/2013/04/national-housing-yajilipua-kuhusu-jengo.html
Shirika la nyumba la Taifa NHC
limekiri kwamba ndio mmiliki wa kiwanja kilichokua kimejengwa jengo la
gorofa 16 ambalo liliporomoka siku kadhaa zilizopita Dar es salaam na
kusababisha vifo vya watu 36 na kujeruhi 18.
Mkurugenzi Mkuu Nehemia Mchechu
amesema kwa kawaida shirika la nyumba limekua likiingia ubia na watu
binafsi wenye uwezo wa kujenga nyumba kama hizo ambapo liliingia ubia na
kampuni ya ujenzi ya RAZA na kusaini mkataba wa kujenga jengo lenye
gorofa 10 tu kwenye eneo hilo ingawa baadae kampuni hiyo iliomba
kubadili mkataba ili wajenge gorofa 16.
Kuhusu umiliki kwa asilimia 25
kwenye jengo lililoporomoka, Mchechu amesema kwa ubia uliokuwepo
walipaswa kupewa asilimia hizo baada ya ujenzi kukamilika na asilimia
nyingine 25 wangepewa miaka kumi baadae kulingana na mkataba na
hawakupaswa kuhusika kwenye gharama zozote wala taratibu za ujenzi.
Namkariri akisema “february 15
2011 ndio walituandikia kwamba wanakusudia kuongeza gorofa zifike 16 na
kwamba wanawasiliana na Mamlaka husika kwa ajili ya kupata vibali hivyo
na wakifanikiwa wangeomba kuongezewa muda wa kumaliza mradi na pia baada
ya kupata kibali wangetutaarifu kwa ajili ya kufanya marekebisho ya
mkataba”
Kwenye line nyingine, NHC
imeunda timu kwa ajili ya kufanya ukaguzi katika miradi yake yote ya
ujenzi wa ubia ili kujihakikishia usalama wa majengo husika.
Post a Comment