RIWAYA: MREMBO ALIYEPOTEA------------1

MTUNZI: Andrew Carlos

MAWASILIANO: 0713133633

SEHEMU YA KWANZA

... Umati wa waumini wa dini ya kikristo ulikuwa unaendelea kumiminika katika kanisa kubwa la Mtakatifu John. Shangwe kubwa ziliendelea kusambaa ndani ya kanisa hilo ikiwa ni msisitizo kwamba waumini wake wameguswa sana na mahubiri yaliokuwa yakiendelea ndani ya kanisa ambayo yalikuwa yakitolewa na mchungaji Joseph. Mmoja wa waumini katika kanisa hilo alikuwa ni Majaliwa na mkewe Juliana. Japokuwa alikuwa ni fundi mabomba na kila siku alitakiwa awe anafanya kazi hata kama ni jumapili, lakini kwake Majaliwa haikuwa hivyo kutokana na kuheshimu sana siku ya jumapili. Aliitenga kama siku muhimu maishani mwake na ya kutubu dhambi zake zote. Upole na ucheshi aliokuwa nao Majaliwa ulizidi kumuongezea marafiki kila kukicha ikiwa ni kanisani mpaka mtaani alipokuwa akiishi. Tatizo kubwa lililokuwa likimuandama Majaliwa ni juu ya mtoto. Pamoja na umri wake kufikia miaka thelathini na tano lakini bado alikuwa hajabahatika kupata hata mtoto mmoja. Alihangaika yeye na mke wake kwenda karibu kila hospitali kujaribu kuangalia pengine mmoja wapo anamatatizo lakini karibu kila hospitali waliyoenda jibu lilikuwa ni hilo hilo kuwa wana uwezo wa kupata mtoto ila kinachotakiwa ni kuvuta subira na kuomba sana kwa mwenyezi Mungu. Ndani ya miezi takribani mitatu tayari mke wa Majaliwa alikuwa ameshanasa ujauzito. Furaha ya ajabu ikamtawala Majaliwa na mkewe Juliana na kuamini kile kilio alichokuwa akikililia kila siku sasa kimepata ufumbuzi. Hakutaka hata kumwacha mke wake abaki nyumbani peke yake mpaka atakapojifungua. Kutokana na kuwa na kipato kidogo alichokuwa akikiingiza kupitia kazi yake ya ufundi mabomba hakikutosha hata kutafuta msichana wa kazi japokuwa pia ilikuwa ni tatizo kubwa kwake kwanza sehemu aliyokuwa amepanga ni ya chumba kimoja. Majaliwa akaendelea kuwa bega kwa bega mkewe mpaka alipofikisha miezi tisa ambayo mke wa Majaliwa alizidiwa na uchungu wa mara kwa mara. “Mume wangu? sijisikii vizuri nakuomba nisidie kunyanyuka hapa!” Aliongea mke wa Majaliwa huku uchungu ukizidi kumzidia hali iliyomfanya Majaliwa atafute usafiri na kumkimbiza hospitali haraka. Woga uliochanganyana na kutetemeka mara kwa mara ukamfanya ajihisi kama mkojo unamtiririka kupitia suruali aliyokuwa amevaa. Muda wote alishikilia mikono yake kwa nguvu nje ya hospitali huku kila muda akionesha ishara kama ngumi juu kwa kusali na kuomba mkewe ajifungue salama hapo hospitali. Jasho jembamba likaendelea kumteremka kupitia kwenye kola ya shati lake huku dhahiri likionesha vifungo kupishana sababu ya haraka aliokuwa nayo ya kumuwaisha mkewe hospitali. Kila mlango wa wodini ulipofunguliwa Majaliwa alikuwa akitetemeka nakuona kama analetewa majibu juu ya maendeleo ya mkewe huko ndani. Hatimaye ndani ya muda mchache akatoka daktari aliyevaliwa mavazi makubwa meupe huku mikononi mwake akilishikilia karatasi na kalamu. “Wewe ndio Majaliwa?” “Ndio mimi dokta, dokta?” Majaliwa aliitikia kwa kutetemeka huku akiendelea kumtolea macho yule dokta. “Twende ofisini kwangu?” Majaliwa akaongozana na yule daktari mpaka ofisini kwake kisha akamkalisha kwenye kiti na maongezi yakaendelea. “Kwanza kabisa nikupe hongera mzee mwenzangu!!” Majaliwa hakutaka kabisa kuamini yale maneno kutoka kwa yule daktari, kwanza akahisi ni ndoto aliyokuwa akiiota kila siku halafu akizinduka inayeyuka. Akajaribu kufumba macho nakufumbua ili kuamini kwamba anachokiona na kukisikia ni kweli kabisa na hayo maneno yanayotoka kwa daktari aliyekuwa amemuita mpaka ofisini kwake au la! “Kwahiyo dokta?, embu niambie mke wangu kajifungua mtoto wa kike au wakiume maana natamani kumuona wee acha tu!!” “Anhaa!, umefanikiwa kupata mtoto wa kike bwana Majaliwa” “Oohh!! Ashukuliwe Mungu, apewe sifa baba yetu aliye Mbinguni, nasema asante sana Mungu umejibu maombi Baba, ulisema kwako hakuna lishindwalo chini ya dunia Baba” Majaliwa akajisahau kabisa kama tayari yupo katika himaya ya hospitali. Akadhania yupo kanisani tena alijihisi yupo kwenye kipindi cha maombi. Akaanza kushukuru taratibu lakini hali ilivyozidi ukichanganya na furaha aliokuwa nayo Majaliwa akajikuta akiitoa sauti kubwa na kali mule ofisini mwa daktari hali iliyomfanya daktari amuondoe ampeleke mpaka alipo mke wake ajionee mtoto wake. Majaliwa alipofika na hapo wodini hali ikamzidia akaanza kutangaza neno la Mungu huku kelele akiziachia karibu wodi nzima kwa kulitaja neno la Mungu na kushukuru kupata mtoto wa kike. Majaliwa akabaki kuwa kama kituko pia kama kivutio katika ile wodi ya wakinamama.Publish PostENDELEA KUSOMA HADITHI HII HAPA>>>>>>>>>>>>>>

Related

HADITHI 8419596209004768612

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item