RIWAYA: WASALIMIE KUZIMU-------1



MTUNZI: Hussein Wamaywa

SIMU: 0755 697335

SEHEMU YA KWANZA

...
Utangulizi

Miaka kadhaa iliyopita, mtu mmoja mtanashati mwenye kiu ya uwendawazimu wa ngono Aitwae Promota Halfan Kigundo alianzisha mashindano ya urembo aliyoyaita Miss Temeke Akademia.

Lengo lake lilikuwa kufanya mapenzi na wasichana wote wataokaojitokeza kupigania taji hilo. Kweli, anafaulu kufanya nao mapenzi na katika hilo, Husna mmoja wa washiriki anapata mimba na kujitoa mashindanoni mapema.

Siku chache kabla ya fainali, rafikie Danny Masimango anamshauri amwingize mashindanoni Nasra Alwatan Dafu (Binti wa kiarabu anayechungwa na baba yake kama malighafi) ili aweze kufanya nae mapenzi kwa kuwa alikuwa mzuri sana.

Halfan anaupokea ushauri huo na kumuingiza mashindanoni, na kwa mbinu za hali ya juu anafaulu kumtongoza, kufanya nae mapenzi na kumjaza mimba pasipo kujua kwamba Nasra anaye mchumba aitwae Saadan huko Oman. Mchumba aliyetafutiwa na baba yake Alwatan Dafu ingawa si chaguo hasa la Nasra.

Siku ya fainali za mashindano ya Miss Temeke Academia, Nasra anajifungua ukumbini watoto mapacha baada ya kunyakua taji. Kitendo kinachowakasirisha wasichana waliotoa penzi kwa Halfan, wanaamua kutoa siri, Halfan anapokea kipigo kutoka kwa mashabiki na wananchi wenye hasira.

ENDELEA SASA>>>>>>

Related

HADITHI 2790279788410142842

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item