RIWAYA: MREMBO ALIYEPOTEA-------- 4

SEHEMU YA NNE

...
Tatizo la kutokuweza kupata mtoto liliendelea sana kumsumbua John Mapunda. Pesa nyingi alizokuwa akizipata kupitia kazi yake ya kusimamia shughuli za urembo hazikuweza kumpa furaha ya nyumba kabisa. Toka alipofunga ndoa na mkewe Janet miaka mitatu iliyopita alizidi kukosa furaha ndani ya nyumba kutokana tatizo la mkewe kutokushika ujauzito. Mwanzoni alijihisi pengine tatizo litakuwa upande wake lakini haikuwa hivyo. Kila hospitali aliyokuwa akiongozana pamoja na mkwewe kujua nani ana tatizo jibu lilikuja pale pale kuwa mkewe John, Janet ni mgumba na kamwe hawezi kupata mtoto. Furaha ya nyumba ikaanza kubadilika siku baada ya siku ndani ya miaka mitatu. John akawa ni mtu wa kulewa na kutembea na wasichana ovyo.
Maisha yake yote sasa akawa ameyahamishia kwenye wanawake. Mwanzoni alifanya kama siri kutembea na wanawake tofauti lakini mwishowe alijionesha dhahiri kutembea na kila mwanamke amtakaye mbele ya mkewe. Hali ile ya John kubadilika kulimuumiza sana mkewe janet. Janet alijihisi ni mtu mkosaji duniani, alijutia ndoa waliyofungishwa kanisani miaka mitatu iliyopita. Uzuri aliokuwa nao Janet na unyenyekevu ilikuwa jibu tosha kwa aliyemuona. Kuimba kwaya kanisani ndio kazi aliyokuwa ameichagua katika maisha yake ya kumtolea Mungu kupitia kipaji alichokuwa nacho. Janet hakuwa na kazi ya maana zaidi ya kujiendesha kwa biashara za mikononi ambapo alikuwa akikopesha kinamama wenzake nguo za watoto na kulipwa baada ya wiki mbili hadi tatu. Kuimba kwake kwaya kulimfanya ajiepushe na mengi japo siri kubwa alimganda moyoni kuwa hana uwezo wa kushika ujauzito. Janet alifanya kila njia kuhakikisha anamuweka mumewe John katika hali ya kutokujisikia tofauti kwa kutopata watoto na akiamini kuwa ipo siku Mungu atawashushia Baraka na watapata mtoto wa maisha, Alihangaika sana kwenda kwenye semina mbali mbali za maombezi na kuombewa sana lakini bado hakuwa na dalili yeyote ya kuondoka ugumba wake.

ENDELEA KUSOMA HAPA

Related

HADITHI 5871877383605334121

Post a Comment

1 comment

Unknown said...

foto hot This is a very good post. Just wonderful. Nice one artis bugil

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item