RIWAYA: WASALIMIE KUZIMU-------------------3

MTUNZI: Hussein Wamaywa

SIMU: 0755 697335

SEHEMU YA TATU Alivunga kwa hili na lile kabla hayajashusha pumzi ndefu na kusema “Oke, hayo tuyaache yashamwagika hayazoleki tena. Vipi kuhusu Saadan, anasema bado anakupenda licha ya yote yaliyotokea yuko tayari pia kukuoa na kuwalea watoto wako iwapo utakubali kwenda kuishi nae Oman. Unasemaje Nasra mwanangu?” Nasra akaachia tabasamu dogo, akageuka na kumtazama Saadan, alikuwa kijana mzuri sana ingawa kwake hakuwa na mvuto kama ule aliokuwa nao Promota Halfan. “Naweza nikakubali baba ikiwa tu atanitekelezea masuala fulani fulani” “Good!” Alwatan Dafu akaruka kwa furaha “Masuala gani?” “Moja nataka umfutie kesi Promota Halfan! Najua unahusika!” “What?” “Eeeh! Hilo la kwanza la pili baada ya kumfutia kesi nataka umuombe radhi kwa kumpiga na kumdhalilisha siku ile ya fainali pale Diamond Jubilee. Aidha nataka umuheshimu na umuhakikishie kuwa hutambughudhi tena na tena umtambue kama mkweo aliyepita na baba wa watoto wangu!” “Mpuuzi!” Alwatan Dafu akanguruma, sharubu zikicheza cheza kwa hasira. Mikono pia ikimcheza cheza. Akaendelea kuongea povu likimtoka mdomoni. “Nasema mpuuzi!! Una wazimu… una wazimu… unawazimu! Sababu ulizotoa sijui masharti hakuna zima hata moja. Nasema utaolewa tu, upende usipende!” “Bila kutimiza hayo siolewi!” Alikuwa Nasra kwa kiburi. “Huwezi kunichezea kama umejizaa mwenyewe sasa utanitambua! Hasira zikamzidi Alwatan Dafu akakunja mikono ya kanzu na kumjongelea mwanae huku akitetemeka kwa hasira. Akamuinua pale kitandani na kumtandika vibao viwili vya nguvu. Nasra akaanza kulia, watoto wake pia wakaanza kulia! Hii haikumfanya Alwatan Dafu asimuinue zaidi na kumkunja vizuri kwa kutumia “Blouse” yake. Mkono wake wenye nguvu ukitua katika shingo la Nasra, Sadaan akamwahi na kumzuia. Nasra akapata nafasi ya kuinuka, akawaifadhi wanae vizuri pasipo kukijali kilio chao halafu akamfuata baba yake, akipiga kelele zilizochanganyikana na kilio. “Saadan! Muache, muache aniue, father kill me, kill me please! Maisha gani haya! Nilishachoka muache aniue ndio niue tu!!” akajitahidi kumnasua lakini Saadan akawa imara.

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item