SITAISAHAU facebook-------15
https://menacotz.blogspot.com/2013/04/sitaisahau-facebook-15.html
MTUNZI: Emmy John P.
MAWASILIANO: 0654 960040
... SEHEMU YA KUMI NA TANO
Zilipita siku nne, kila siku nilikuwa napitia barua pepe yangu kutazama
kama kuna majibu yoyote kutoka kwa Dokta Davis lakini mambo yalikuwa
tofauti Davis hakupiga simu wala hakujibu ujumbe niliomtumia.
Nilijiuliza je? Nimpigie simu ama niendelee kuvuta subira. Hali hiyo ya
kungoja sana ikanitia mashaka, kumpigia simu pia nikasita kwa kukumbwa
na maswali mengi. Kama hajaisoma ile e-mail itakuwaje? Na kama ameisoma
pia nilitegemea maswali mchanganyiko ambayo yangeweza kunitia katika
majaribu ya kumweleza Davis juu ya ile mimba ya kimaajabu! Jambo ambalo
sikutaka kabisa litokee. Nikaendelea kuwa kimya!
Siku zikasonga mbele. Amani finyu moyoni! Maria sasa akawa kama ndugu yangu, tuliendelea kuishi wote.
SASA ENDELEA KUSOMA HADITHI HII
Post a Comment