SIMBA TV YAINGIA MKATABA WA MILLION 331 NA AZAM TV

KAMPUNI ya mpya ya Habari nchini, Azam Media Group, leo
imeingia Mkataba wa miaka
mitatu wenye thamani ya Sh.
Milioni 331 na klabu ya Simba ya
Dar es Salaam kwa ajili ya
kurusha kipindi maalum cha
klabu hiyo, kitakachojulikana
kama Simba TV kupitia kituo
kipya cha Televisheni, Azam TV.
Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj
Ismail Aden Rage, kwa pamoja na
Katibu, Evodius Mtawala na
Mjumbe wa Baraza la
Wadhamini, Hamisi Kilomoni
waliiwakilisha klabu hiyo katika
utiaji saini wa Mkataba huo
mnono kwenye ukumbi wa Kibo,
jengo la PSPF, Dar es Salaam.
Upande wa Azam uliwakilishwa
na Mkurugenzi Mkuu, Abubakar
Bakhresa, Meneja Mkuu, Said
Mohamed na Mwanasheria, Shani
Christoms ambao waliikabidhi
Simba SC hundi za fedha hizo
kwenye hafla hiyo.
Meneja wa Azam Media, Mzee
Said alisema kwamba Mkataba
huo ni mwanzo tu, lakini
kampuni hiyo imejipanga kusaidia
zaidi soka ya Tanzania kwa
kuingia mikataba mingi yenye
manufaa kwa mchezo huo nchini.
Alhaj Rage, pamoja na
kuwashukuru Azam Media kwa
Mkataba huo mnono, alisema
klabu inategemea kujikomboa
zaidi kiuchumi kutokana na
mikataba ya udhamini kama hiyo
na muda si mrefu wataingia
mikataba mingine itakayokuza
zaidi pato la klabu.
“Nimesikia pia mnataka kununua
haki za Televisheni za Ligi Kuu ya
Tanzania Bara, mimi nasema
karibuni na katika hilo, natoa
angalizo, mkinunua haki za TV za
Ligi Kuu, naomba mtoe fungu
sawa kwa kila klabu, hakuna
kubagua eti huyu apate kidogo,
yule apate zaidi, hapana,”.
“Lazima mpira wa miguu katika
nchi hii maendeleo yafike kila
sehemu na tuondoe ubinafsi wa
kujifikiria eti sisi Simba ndiyo
tupate zaidi, hapana. Hiyo si haki,
lazima na zile klabu ndogo pia
nazo zinufaike sawa na sisi kwa
kuwa tunacheza ligi
moja,”alisema Rage ambaye pia
ni Mbunge wa Tabora Mjini
(CCM).

CHANZO: BIN ZUBEIRY

Related

SOCCER 3565075749123120797

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item