HAWA NDIO WALIOTISHA KWENYE USAJILI JANA

Baada ya Arsenal kumnasa Ozil,  Manchester United kumnasa Fellain, na Everton kumnasa Lukaku zimekuwa ni habari za usajili zilizotisha zaidi jana usiku kwa upande wa ligi kuu ya Uingereza kwenye kufunga dirisha la usajili jana Usiku. 

OZIL KWENDA ARSENAL;

Mashabiki wa Arsenal hawakuwa na imani kabisa na kocha wao baada ya kocha huyo kuonekana wanasuasua kwenye dirisha la Usajili, Wenger aliwadhihirisha mashabiki wa timu hiyo kuwa ana uwezo wa kuasjili wachezaji wa kiwango cha juu na kwa pesa nyingi na kama alivyofanya kwa kumsajili Mesuit Ozil kutoka Real Madrid kwa ada ya uhamisho iliyofunja rekodi ya Klabu hiyo kwa kutoa kitita cha £42.5 mil. hii imewapa furaha mashabiki wa Arsenal na kusahau machungu yote ya kocha huyo anayedaiwa kuwa mbahili.

FELLAINI KWENDA MANCHESTER UNITED

Baada ya Meneja wa Manchester United kushindwa kumsajili Fabrigas kutoka Barcelona, Moyes alielekeza makali kwa Mbeligiji Maourine Fellain, Leighton Baines (EVERTON), De Rossi ( AS ROMA) na ANDERS HERRERA wa Athletico Bilbao, hata hivyo Herrera alishindwa kujiunga na MANCHESTER UNITED baada ya nchi hiyo kutaka Manchester iongeze
6mil, kwenye ada ya uhamisho ya  €36mil. Lakini Manchester United ilitaka kumnasa beki wa Real Madrid Fabio Contreao, ila klabu hiyo ilishindwa kwa kuchelewa kukamilisha taratibu za uhamisho huo. lakini Moyes hakukata tamaa maana kabla dirisha halijafungwaaliweza kuinasa saini ya Mbeligiji aliyekuwa anakipiga Everton , Fellain kwa ada ya uhamisho ya £27 mil. Hii imekuwa faraja kwa Mashabiki wa United kwa kuwa wamekuwa na tatizo la kiungo wa kati tangu kuondoka kwa Roy Kean.

LUKAKU KWENDA EVERTON

Everton baada ya kumpoteza Fellain waliweza kuwasajili wachezaji wawili ambao ni Romelu Lukaku kutoka Chelsea kwa Mkopo wa mwaka mmoja. juku ikiweza kumnasa pia kiungo  James McCarthy ili kuziba pengo la Fellaini.



Related

USAJILI 5520134926259350445

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item