OKWI STOP KICHEZEA YANGA

Huku Ligi ya kandanda nchini Tanzania ikitarajia kuanza mzunguko wake wa Pili Mwishoni mwa juma hili, Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) limesimamisha usajili wa mshambuliaji Emmanuel Okwi
kutoka Uganda katika timu ya Yanga wakati likisubiri ufafanuzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana leo (Januari 22 mwaka huu) kupitia
masuala mbalimbali imesimamisha usajili huo
baada ya kubaini kuwa Okwi aliruhusiwa kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali maalumu kutoka FIFA.

Okwi ambaye aliingia mgogoro na klabu yake ya Etoile du Sahel ya Tunisia aliruhusiwa na FIFA kuchezea SC Villa kwa kibali maalumu (provisional permit) cha miezi sita ili kulinda kiwango chake wakati suala lake dhidi ya Etoile
du Sahel likishughulikiwa na shirikisho hilo la kimataifa.
Katika FIFA kuna kesi tatu kuhusiana na suala la mchezaji huyo. Wakati Okwi ameishitaki
klabu hiyo FIFA kwa kutomlipa mshahara, Etoile du Sahel imemshitaki mchezaji huyo kwa
utoro. Nayo Simba imeishitaki Etoile du Sahel kwa kushindwa kuilipa ada ya mauzo ya mchezaji huyo ambayo ni dola za Marekani
300,000. Hivyo, TFF imeiandikia FIFA kutaka kujua iwapo mchezaji huyo anaweza kucheza Ligi nchini
Tanzania wakati Etoile du Sahel ikiwa.imefungua kesi katika shirikisho hilo la kimataifa ikidai Okwi bado ni mchezaji wake.
Emmanuel Okwi ambaye aliwahi Kuichezea Simba kabla ya kuuzwa kwenye Klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia,alikaribishwa kwa
mbwembwe na hoi hoi nyingi wakati alipokuja kuanza kuichezea Yanga mwishoni mwa mwaka
uliopita ambapo katika mechi dhidi ya Simba alifunga bao 1 la kufutia machozi WAKATI Yanga ilipobamizwa bao 3-1 na Simba katika Mechi maalum kati ya watani hao wa jadi katika Soka la Tanzania.

SOURCE::BBC

Related

YANGA 3682717542181797629

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item