Gary Lineker; MAN U WATASHINDA KAMA BARCA WATACHEZA VIBAYA


GARY LINEKER nahodha wa zamani wa barca na timu ya taifa ya england


Aliyekuwa nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya England Gary miaka ya 80 ameibuka na kuzungumzia mechi ya fainali ya UEFA kati ya Man U na Barca itakayofanyika jumamosi hii kwenye uwanja wa wembly England., Gary alidai kuwa Man u wanaweza kushinda endapo Barca wakicheza vibaya siku hiyo ya fainali. Gary ammbaye ameichezea Barca kati ya mwaka 1985 na1986, amesema Barca ni timu nzuri na inapewa nafasi kubwa ya kutwaa  taji hilo la ushindi lakini wanapaswa kuwa makini maana Man u wanachezea nchini kwao japokuwa Barca ndio wenyeji wa mchezo huo. pia alizidi kusema kuwa kwa soka la sasa Barca ndio timu inayoogopwa sana duniani ukiacha miamba mingine ya soka kama AC milani, Real Madrid na Inter milan. Gary aliyasema haya wakati akihijwa na kituo cha radio kinachomilikiwa na BBC cha radio 5. pia kutokana na kile wapenzi wa soka duniani wanakipenda kupata historia za mechi kubwa za timu zinazokuta hapa chini nakuletea historia ya mechi za man u na barca

BARCELONA v MAN UTD
  • 7 Mar 1984 Barca 2-0 Man Utd
  • 21 Mar 1984 Man Utd 3-0 Barca
  • 15 May 1991 Man Utd 2-1 Barca
  • 19 Oct 1994 Man Utd 2-2 Barca
  • 2 Nov 1994 Barca 4-0 Man Utd
  • 16 Sep 1998 Man Utd 3-3 Barca
  • 25 Nov 1998 Barca 3-3 Man Utd
  • 23 Apr 2008 Barca 0-0 Man Utd
  • 29 Apr 2008 Man Utd 1-0 Barca
  • 27 May 2009 Barca 2-0 Man Utd
wamekutana mara kumi wametoka sare mara nne na kila mmoja ameshinda mara tatu. sasa atakayeshinda jumamosi atakuwa amemzidi mwenzake na si hivyo tu pia atakuwa ametwa kombe hilo mara nyingi zaidi mwenzake maana wote  wametwaa taji hilo mara tatu.


Related

free to all 7272988937335088185

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item