Mubarak ashinda kesi ya rufaa
https://menacotz.blogspot.com/2013/01/mubarak-ashinda-kesi-ya-rufaa.html
Rais wa zamani wa Misri, Hosni
Mubarak, ameruhusiwa kufanyiwa kesi nyengine kwa makosa ya kutozuwia
mauaji ya waandamanaji mamia kadha wakati wa ghasia zilizomuondoa
madarakani.
Mahakama ya rufaa mjini Cairo, baada ya kikao kifupi, yalitoa amri hiyo ya Bwana Mubarak kufanyiwa kesi nyengine.
Mwezi wa Juni mahakama yalitoa hukumu ya kifungo
cha maisha kwa Rais Mubarak kwa hatia ya kuwa na dhamana ya mauaji ya
waandamanaji yaliyofanywa na askari wa usalama ambao wakijaribu kuzima
ghasia za mwaka wa 2011.
Mkuu wa usalama wa Bwana Mubarak, Habib el-Adly,
ambaye anatumika kifungo cha maisha kwa mashtaka kama hayo, piya
atafanyiwa kesi
CHANZO: BBC
CHANZO: BBC
Post a Comment